Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. George Fuime imefanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Sekta ya Afya na Elimu inayotekelezwa maeneo tofauti hapa Wilayani ikihusisha Umaliziaji wa Vyumba viwili vya madarasa vya madarasa kwa shule ya Msingi (ilolo,Nzugilo,Vikundi na Mwenzele),Umaliziaji wa vyumba vya Maabara kwa Shule za sekondari (Ihala,Kimagai na Matomondo), Ujenzi wa Zahanati katika vijiji(Mkoleko,Kiboriani, na Mlembule) pia ujenzi wa matundu ya vyoo kumi na mbili Shule ya Sekondari Matomondo.
Kamati ilibaini nguvu kazi ndogo zinazochangiwa na wananchi katika Miradi hiyo, Taratibu za Manunuzi kuchelewa na baadhi ya Taasisi kama Shule na Zahanati kuwa na maeneo yasipimwa na kutokuwa na hati miliki.Kamati ikiongozwa na Mhe Fuime imemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa Ndug Julieth Ntuku kuwaelekeza watendaji kuzingatia taratibu za manunuzi na kuzielekeza kamati za ujenzi za vijiji utaratibu unaofaa katika manunuzi kuepuka kutumia muda mwingi katika manunuzi ya vifaa,kuzingatia ubora wa majengo na kuhakikisha maeneoya Shule na Zahanati yanapimwa na kutafutiwa hati.Kaimu Mkurugenzi ameishukuru kamati kwa kuitembelea Miradi hiyo na kuahidi kutekeleza maagizo yote ya Kamati na kuyafikisha Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.
Mhe.george Fuime Mwenyekiti wa Halmashauri (aliyetangulia mbele) akiongoza wajumbe wa kamati kukagua umaliziaji wa vyumba viwili vya Maabara katika shule ya Sekondari Kimagai.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.