Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Josephat P. Maganga Anawatangazia Wananchi wote wa Wilaya ya Mpwapwa kuwa tarehe 31 Julai, 2021 Siku ya Jumamosi asubuhi Mwenge Maalum wa Uhuru kwa mwaka 2021 unatarajiwa kuwasili eneo la Chamnye kata ya Mazae saa 1:00 asubuhi, utapokelewa kutoka Wilaya ya Kongwa. Mwenge huo unatarajiwa kukimbizwa takribani Kilometa 173 na kuzindua, kutembelea na kuweka mawe ya msingi katika Miradi mitano, na baadae utakesha kata ya Mtera katika Shule ya Msingi Mtera. Katika eneo la Mkesha kutakuwa na Maonyesho ya Shughuli za TEHAMA, LISHE, TAKUKURU, MALARIA, UTHIBITI WA MADAWA YA KULEVYA na VVU/UKIMWI.
Miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni kama ifuatayo:-
1. Kikundi cha Wajasiriamali National Housing, kilichopo katika Kata ya Mpwapwa Mjini eneo la National Housing.
Katika mradi huo Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kutembelea na kukabidhi pikipiki kumi (10) zilizokopeshwa na Halmashaui ya Wilaya ya Mpwapwa kwa wajasiriamali.
2. Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Miembeni, Kata ya Mpwapwa Mjini
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuzindua daraja kubwa na la kisasa lililojengwa katika Mto unaopita katikati mwa Mji wa Mpwapwa ambao unatenganisha Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa na Soko Kuu la Mpwapwa.
3. Mraji wa Maji katika Kijiji cha Iramba kata ya Rudi.
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuzindua Mradi huo ambapo kwa miaka mingi wananchi wa kijiji hicho walikuwa na uhaba wa maji na sasa wamejengewa mradi maji bomba.
4. Mradi wa Madarasa Mawili katika Shule ya Sekondari Ikuyu kata ya Luhundwa
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa Kuzindua Mradi huo.
5. Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Mtera kilichopo katika Kijiji cha Mtera kata ya Mtera.
Katika kituo hicho Mwenge wa Uhuu unatarajiwa kuweka jiwe la Msingi.
Hivyo Mkuu wa Wilaya Anawaomba wananchi wote Kujitokeza kwa Wingi katika kushiriki katika Mapokezi, Kukimbiza na Kukesha katika Siku hiyo ya Mwenge wa Uhuru.
Pia amesisitiza Kila mwananchi kuchukua Tahadhari ya Kujikinga na Ugonjwa wa Virusi Vya Korona 19 (UVIKO19).
........Mwenge wa Uhuru 2021, Oyeeee.......
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.