Katika Kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya Kwanza kilichofanyika tarehe 13.12.2017, pamoja na mambo mengine kulikuwa na nasaha za wawakilishi wa wajumbe wa ALAT (M) ambao ni wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya ya Kongwa, Bahi , Chamwino pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Akitoa nasaha katika Baraza hilo la Madiwani Mwenyekitii wa ALAT Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa kwa kuendesha Baraza vizuri. Alisema yeye pamoja na wenzake wamejifunza matumizi mazuri ya muda na mtiririko wa agenda. Baraza hilo lilifanyika kwa muda wa masaaa mawili tu huku wenyeviti wa kamati za kudumu wakitekeleza wajibu wao vyema wa kuwasilisha na kutoa ufafanuzi wa taarifa za kamati wanazo zisimamia.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.