Mkuu wa Wilaya Josephat Maganga amekabidhi Pikipiki kumi(10) kwa kikundi cha Umoja National Housing kinachotoa Huduma za usafiri wa ndani(Bodaboda) zenyethamani ya Tsh 24,590,000 ikiwa ni fedha ya asilimia kumi (10%) ya Mapato ya Halmashauri inayotengwa ka ajili ya Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu. ukiwa ni mkopo usio na riba chini ya usimamizi wa Ndugu Khamlo Njovu Mkuu wa idara ya Maendeleo na Vijana. Pia Mhe Maganga amewasisitiza wanakikundi hao kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujiongezea kipato, kurejesha mkopo huo na kuruhusu wengine kukopa,kutunza pikipiki walizokabidhiwa na kuzingatia sheria za barabarani. Mkuu wa Idara ya Maendeleo na vijana amewashukuru watu wote kwa kuhudhuria na kuwasisitiza kikundi cha National Housing kuhakikisha wanatunza pikipiki hizo nakurejesha mkopo huo kwa wakati.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo na Vijana Ndugu Khamlo Njovu akisoma majina ya wanakikundi ili Mgeni Rasmi Mhe.Mkuu wa Wilaya Josephat Maganga (watano kutoka kushoto) aweze kuwakabidhi kadi za Pikipiki hizo.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.