Tume ya Utumishi wa Umma Serikalini imefika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa leo Agosti 18,2025 .
Kazi kubwa ya Tume ya Utumishi wa Umma ni kufuatilia na kusimamia uendeshaji wa shughuli za Rasilimali watu katika Taasisi za Umma na kuhakikisha kuwa Utumishi wa Umma unaendeshwa kwa mujibu wa Sheria.
lengo kuu la Tume ya Utumishi wa Umma ni ukaguzi wa kimaadili kwa watumishi wa Umma.
-Ukaguzi wa ajira mpya na za mkataba
-Upandishwaji wa vyeo kwa mujibu wa Sheria,muongozo, taratibu na kanuni.
-Nafasi za Madaraka
-Likizo ya mwaka na uzazi
-Eneo la mafunzo na majitaji ya watumishi
-Uzingatiaji wa Maadili na Nidhamu na fidia za ajali na mafao yatokanayo na kazi
Tume ya Utumishi wa Umma imeanzishwa mwaka 2002,na kwa mujibu wa maboresho mapya ya mwaka 2004 inaelekeza majukumu mbali mbali kama vile
-Kufanya ukaguzi
-Kumshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutekeleza majukumu yake aliyopewa kwa mujibu wa Ibara ya 36 ya Katiba ya Jamhuri ya
-Kuwa na mamlaka ya rufani.
Timu hiyo ya ukaguzi wa kimaadili kutoka Tume ya Utumishi wa Umma itafanya ukaguzi wake kwa siku tatu kuaniza Agosti 8-10,2025 katika Halmashauri ya Mpwapwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.