Kundi la tembo wapatao 20 wamekatiza katika makazi ya watu na kujeruhi mkaazi mmoja aliyejulikana kwa jina la Japhet Lechipya (28) wa kijiji cha Idilo katika kata ta Mazae. Tukio hilo limetokea kufuatia jaribio la mjeruhiwa kujaribu kuwapiga picha tembo hao waliokuwa wanapita katika makazi hayo.inasadikika kuwa tembo hao wametokea katika mbuga za mikumi.Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama Mhe. Jabir shekimwer amelielezea tukio hilo kuwa tembo hao wametokea katika wilaya ya jirani ya Chamwino na inasadikika kuwa wametoroka kutoka mbuga ya Mikumi. Aidha Mhe.Shekimwer ametoa wito kwa wananchi kuacha kuwasogelea Tembo hao na kuwachokoza ili kuepuka madhara kwakuwa wanyama hao hawapendi kelele.
Daktari wa Wilaya ya Mpwapwa Dr. Said Mawji amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo ambapo amekiri kumpokea mgonjwa mmoja ambaye alijeruhiwa vibaya lakini kwa kushirikiana na madaktari waliopo wameweza kumtibu majeruhii huyo na hali yake inaendelea vizuri.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.