(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) leo limetembelea miradi mbalimbali katika Wilaya ya Mpwapwa kwa ajili ya kuandaa Makala Maalum kuhusu miradi inayotekelezwa katika wilaya hiyo. Miradi iliyotembelea ni pamoja na barabara ya kiwango cha lami ya Mpwapwa mjini, Mradi wa Maji Kibakwe, Kituo cha Afya Kibakwe, Shule ya Sekondari Kibakwe, Shule ya Sekondari Mpwapwa, Mradi wa Kitalu cha Miche ya Mikorosho, Katika kutembelea miradi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri ameambatana na wataalam toka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa pamoja na waandishi wa Habari toka TBC wakiongozwa na Ndug. Elisha Elia.
Aidha miradi iliyotembelewa na TBC ni kama ifuatayo:
1. Mradi wa Uzalishaji wa Miche ya Mikorosho katika Kijiji cha Ilolo.
Wilaya ya Mpwapwa imeanza kujikita katika kilimo cha korosho tangu mwaka 2017 na hiki ni moja ya vituo vya uzalishaji miche katika wilaya hii ambapo kwa mwaka huu kila kata ina kitalu angalau kimoja cha kuzalisha miche kama hii. Ameeleza Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Ndug. Maria Leshalu. Pia Leshalu ameongeza kuwa "Miche hii huzalishwa na vikundi vya wakulima waliowezeshwa kupata elimu ya namna bora ya kuotesha miche ya Mikorosho ambapo pia wanalipwa na bodi ya korosho kwa kazi hii. Kwa mwaka jana takribani Tsh. 283,000,000.00 ziligawanywa kwa vikundi na mtu mmoja mmoja waliozalisha miche ya mikorosho katika wilaya hii."
Akielezea malengo ya kuanzisha kilimo cha zao la korosho katika Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. Shekimeri kuwa "Kwanza: ni Kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika Kukijanisha Dodoma, kauli mbiu iliyoziduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan, Pili: Korosho ni zao mkakati kwa ajili ya kuinua kipato cha mwananchi au mkulima mmoja mmoja ua kikundi, tatu: Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa itakusanya mapato kupitia zao hili na kufanya Halmashauri kuongeza na kujihimarisha katika mapato yake ya ndani, nne: zao la korosho linajibu changamto ya Tanzania ya viwanda kwa maana kupitia zao hili tutapata viwanda vya kubangua na kusindika korosho, na tano: agenda ya korosho inatarajia kutoa ajira kwa wananchi wa Mpwapwa tangu kuotesha miche, kupanda, kupalilia, kuvuna, kubangua na hata kuuza korosho. Katika hatua zote hizi nguvu kazi inahitajika na hivyo ndio ajira zitapatikana".
Ndug. Maria Leshalu (kushoto) akimuelezea Mwandishi wa Habari wa TBC Ndug.Elisha Elia (kulia) juu ya kuandaa vitalu vya miche ya mikorosho
2. Mradi wa Barabara ya Lami
Waandishi wa Habari wa TBC wamepata fursa ya kutembelea na kupata maelezo ya kina juu ya barabara ya kiwango cha lami iliyopo Mpwapwa Mjini kuanzia Mtaa wa Mwanakianga hata Mtaa wa Hazina kupitia Mpwapwa Mjini.
Barabara ya lami iliyopo Mpwapwa Mjini
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.