Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Paul Mamba Sweya leo amepokea msaada wa vifaa vya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa COVID19 unaosababishwa na virusi vya Corona.
Msaada huo wa vifaa vikiwemo vitakasa mikono, sabuni na gloves vyenye thamani ya Tsh 200,000/= vimetolewa na Ndugu. Amina Nkumbi Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) tawi la Wilaya ya Mpwapwa.
Ndugu. Amina amesema kuwa "Chama cha wafanyakazi wa Serikali za Mitaa tawi la Mpwapwa kimeona kuna haja ya kuchangia vifaa hivi vitakavyotukika na wananchi katika maeneno yenye mikusanyiko pamoja na maofisini"
Naye, Mkurugenzi wa Wilaya ya Mpwapwa amekishukuru chama cha TALGWU kwa msaada huo na ameahidi kuvigawa vifaa hivyo katika maeneo ya Vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo mengine ya mikusanyiko.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.