Maadhimisho ya siku ya Unawaji Mikono duniani Kiwilaya yameadhimishwa Mei 5,2024 katika kata ya Kibakwe Wilaya ya Mpwapwa katika kituo cha Afya Kibakwe,yakiwa na kauli mbiu isemayo "Usafi wa mikono ni nyenzo ya kutoa huduma ya afya na kuzuuia maambukizi ya magonjwa."Siku ya unawaji mikono mwaka 1940 nchini Marekani ikiw na Lengo la kuhimiza usafi wa mikono duniani kote na kwa watu wote.
Katika Maadhimisho hayo Mhe.Richard Maponda kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ambae ndie Mgeni rasmi amewataka Wananchi waache tabia ya kunawa mikono kimazoea na kuwasisitiza kuendelea kudumisha usafi wa kunawa mikono kwa sababu ya mahitaji mbalimbali ya kikimwili yanayohitaji usafi wa kunawa mikono.
Pia amtaka Afisa Afya ahakikishe maeneo yote ya wananchi wetu wote katika vyoo vyao Yawe na vyombo tiririka kwa ajili ya kunawa mikono,na kutoe elimu baadhi ya sehemu zenye mkusanyiko wa watu ili kuweza kuimarisha suala zima la unawaji mikono.
Katika maadhimisho hayo Shule kumi na tano za Wilayani Mpwapwa zimetunukiwa vyeti vya kufanya vizuri katika masuala yaa usafi na kupata zawadi za dawa za kusafishia na mifagio,vilevile Shule ya Msingi Kibakwe na Idunda walipata zawadi za taulo za kkike pamoja na sabuni za kunawiya mikono na kuogea.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.