Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi H Ally leo Septemba 26,2025 amekabidhi baiskeli za wahudumu wa afya ngazi ya jamii kwa lengo la kuwasidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo amesema dhumuni kubwa la kupatiwa baskeli ni kuzitumia katika utoaji wa elimu ,kufuata na kufuatilia wagonjwa,kuhamasisha matumizi ya huduma za afya na kutoa taarifa za kitakwimu kwa wakati.
"Lengo la kupatiwa vitendea kazi hivi ni kuweza kuwafikia na kuwafatilia wagonjwa wetu wa maeneo ya mbali,lakini pia kuielimisha jamii kuhusu afya ya uzazi,lishe pamoja na magonjwa ya kuambukiza
"Ni wajibu wetu kuwatembelea na kufuatilia wagonjwa wa VVU,kifua kikuu,kisukari nakadhalika pamoja na kuwahamasisha kutumia vituo vya afya kwa ajili ya chanjo,kliniki ya mama na mtoto na uzazi wa mpango".Amesema Bi Mwanahamisi
Halikadhalika Mkurugenzi Mtendaji amewakumbusha wahudumu wa afya ngazi ya jamii ifikapo Octoba 29,2025 wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura.






Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.