Timu ya Wataalam kutoka Mradi wa Reli ya Treni ya Mwendokasi (SGR) leo imefika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuja kutambulisha Miradi na program mbalimbali zitakazotekelezwa katika Wilaya ya Mpwapwa kwenye vijiji vinavyopitiwa na Mradi wa SGR.
Miradi na program zitakazotekelezwa na SGR ni pamoja na Ujasiriamali, Utunzaji wa fedha, Uzalishaji mali na kusomesha vijana katika chuo cha VETA katika fani mbalimbali. Program hizo itadumu takribani kwa muda wa miaka 10.
Wakuu wa Idara wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa SGR mara baada ya kumaliza kikao, (watatu kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa).
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.