Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary S Senyamule amewatembelea Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtera Dam kufuatia maafa yalijotokea Novemba 12,2025 ya kuunguliwa na moto Bweni lao na kupoteza kila kitu.
Kufuatia tukio hilo,Uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa iliwalazimu kufanya utaratibu wa kuwahamisha wanafunzi hao na kuwagawanya kwenye Shule mbili ya Mazae na Kimagai "A" ili waweze kuendelea na masomo yao kama kawaida.
Mhe Senyamule aliwatembelea Wanafunzi waliopo Shule ya Sekondari Mazae Novemba 13,2025 akiwa ameambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt Khatibu Kazungu,Kamati ya Usalama Mkoa na Afisa Elimu Mkoa,ambapo walitoa baadhi ya Mahitaji ya wanafunzi hao waliofikwa na majanga hayo ya kuuguliwa na moto ikiwa lengo ni kuwasidia kwa baadhi ya mahitaji na kuweza kuendelea na masomo yao bila kuwepo changamoto yoyote.
Akizungumza na Wanafunzi hao Mhe Senyamule amesema jambo jema la kumshukuru Mungu ni kwamba hakuna maisha ya mwanafunzi yoyote yaliyopotea zaidi ya vitu tu ambavyo vinaweza kutafutwa,ila uhai wa mtu hauwezi kutafutwa wala kupatikana sehemu yoyote.
"Jambo la kumshukuru Mungu ni kwamba hakuna kati yenu ata mmoja aloungua wala kupata madhara zaid ya kuunguliwa vitu tu, vitu vinatafutwa watu hawatafutwi" amesema Mh Senyamule
Hata hivyo,Mhe Senyamule ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa kwa jitihada zao walizochukua kuhakikisha Wanafunzi hao wa kidato cha tano na cha sita wanaendelea kipata masomo yao kama kawaida.
Vilevile kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe Dkt Sophia Mfaume Kizigo amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa akali hiyo ya moto imesababishwa na hitilafu ya umeme iliyojitokeza kwa miundombinu ya nishati iliyomo ndani ya jengo hilo.








Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.