Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar K. Mmuya amefanya ziara ya kukagua miradi mbali mbali ya kimaendeleo inayorajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru ambao unatarajiwa kupokewa Aprili 27,2025.
Miradi iliyokagulia ni pamoja na Kilimo,Afya,Miundombinu,vijana Utawala na Maji.
Aidha Bw.Mmuya amewapongeza kwa hatua mbali mbali zilizofikiwa katika miradi na kusisitiza kufanyia kazi maboresho waliyoyatoa ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati.
Akizungumza katika ziara hiyo katibu Tawala Mkoa amewataka Wananchi kuwa walinzi wazuri wa miradi yote inayotekelezwa na Serikali ili iweze kudumu na kuweza kunufaika kwa muda mrefu.
Ziara hiyo imefanyika Aprili 04, 2025 katika Wilaya ya Mpwapwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.