Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi mradi wa Reli ya Mwendokasi(SGR) Katika ghafla iliyofanyika Mkonze Jijini Dodoma
na kuzungumza na Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa reli ya mwendokasi
Akizungumza Agosti 1,2024 Jijini Dodoma amesema mrdi huo ambao umetekelezwa kwa gharama kubwa na umejengwa kwa vciwango vya juu utaleta matumaini mapya katika sekta ya usafiri nchini.
Ametaja kwa mtiririko majina ya mtiririko za reli hiyo kwa kueleza kuwa kituo cha Dar es salaam kitaitwa jina la Magufuli,Kituo cha Morogoro kitaitwa Kikwete,Kituo cha Dodoma kitaitwa Samia,wakati kituo cha Tabora kitaitwa Mwinyi,kituo cha Shinyanga kitaitwa Abeid Karume,Mwanza kitaitwa Nyerere na cha Kikoma kitaitwa Mkapa.
Hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali,wawakilishi wa sekta binafsi na wananchi,walitumia fursa hiyo kusifia juhudi zilizowekwa na Serikali kuhakikisha mradi unakidhi viwango vya kimataifa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.