Makamu wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mpwapwa Mjini pamoja na wajumbe wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango wakiwa katika ukaguzi na tathmini ya athari ya mafuriko zinazoletwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hii. Katika ziara hiyo Makamu mwenyekiti ameambataba ba wakuu waidara mbalimbali ili kukagua na kunaona namna ya kuwasaidiwa wananchi wanaoishi kandokando mwa korongo linalopita Mpwapwa mjini ambalo kwa miaka mitatu mfururulizo limekuwa litanuka na kusababusha nyumba zilizopokandokando yake kubomoka na wengine kuyahama makazi yao.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Mpwapwa mjini katika Mtaa wa Majengo, Mhe. Fuime amesema kuwa 'Kwa sasa mvua inanyesha nchi nzima na hivyo serikali inashughulikia majanga ya mafuriko katika sehemu mbalimbali ila ninyi wananchi mnatakiwa kuanzisha jitihada ya kukabiliana na halii kwa kuanzisha michango na kuleta mawe na mchanga ili Serikali iweze kuleta saruji na wataalam wa kujenga gabioni ili kukinga maji ya korongo yasiweze kuleta madhara makubwa".
Kwa upande wao wananchi wamesema wameshakusanya mawe na mchanga wa kutosha wanaomba msaada mawe hayo yaweze kufikishwa katika sehem husika kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa kuzuia korongo kupanuka na kuathiri makazi yao.
Kufuatia jitihadi hizi za wananchi; Mhe. Fuime amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Paul M. Sweya kuleta lori la kubema mawe na mchanga ili kuleta eneo husika. Pia Mhe. Fuime amemuagiza Ndugu. Sweya kufuatilia ahadi ya mifuko 100 ya saruji aliyohaidi kutoa Mhe. George Lubeleje Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa kwa ajilia ya ujenzi wa kuta za kuzuia pananuka kwa korongo hili.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.