Mradi wa NORISH umeanzwa kutekelezwa Wilaya ya Mpwapwa mwishoni mwa mwaka 2024 katika Kata 11 vijiji 39 ukiwa chini ya wafadhili wa Nchi ya Norway kupitia Shirika lake la maendeleo NORAD na kutekelezwa na wadau wanne ambao ni Shirika la NVS,Shirika la Farm Afican,RECODA na MARC
Lengo la mradi huu ni kuwawezesha wakulima madogo kuwa na usalama wa chakuka, lishe bora,na kilimo himilivu juu ya mabadiliko ya tabia ÿa Nchi, jumla ya wahudumu wa afya na wakulima viongozi 78 walipatiwa mafunzo ya mradi huo.
ameelezea mafanikio mbali mbali yaliyopatikana juu ya mradi wa NORISH ikiwemo kuelimisha juu ya utengenezaji wa bustani za nyumbani,
Kuunganisha wakulima na kapuni za pembejeo za kilimo, kuanzisha vikundi vya kilimo vikiwa na Wananchi 2,100 wakiume 970 na wa kike 1,130,kuanzisha mashamba darasa na kujifunza kwa vitendo,na pia kugawa pakti 430 za mbegu za mbogamboga kama vile chainizi,mchicha,bamia,spinachi na saro.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya Ndg Obert Mwalyego ambae ji Afisa Tarafa wa Mpwapwa Mjini amesema "huwezi ukafanya vizuri kama huna chanzo cha mbegu bora , wakulima waache kulima kwa mazoea ili kuweza kupata mazoa yaliyo bora."
Pia amesisitiza lazima kufuatwe utaratibu na kanuni za wataalamu wa kilimo.
Mwisho ametoa wito kwa wakulima hao waliopata ujuzi juu ya lishe bora wausambaze ujuzi huo kwa wengine wasikae nao peke yao,na pia mbegu za kilimo zifike kwa wakati na sio kutumia mbegu za mazoea walizozikuta kutoka kwa mababu zao.
Siku ya Wa kulima Wilayani Mpwapwa iliuofanyika kijiji cha Chogola kata ya Massa imebebwa na Kauli mbiu isemayo
"Usalama wa chakula, lishe bora na kilimo endelevu"
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.