Naibu Waziri wa Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deo Ndejembi akiwa katika ziara yake ya kutembelea Halmashauri za Wilaya mbalimbali hapa Nchini, amefika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa na kusikiliza kero zao juu ya utumishi wa umma na kuzitatua hapo hapo. Pamoja na kutatua kero Mhe. Ndejembi alitaka kujua kama watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wanafuata kanuni na miongozo ya utumishi wa umma ikiwemo ni pamoja na mipango kazi na OPRAS. Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa alipoulizwa kama watumishi wana mipangokazi na OPRAS alikiri kuwa ni kweli watumishi wachache tu wenye OPRAS na mipango kazi na hivyo alihaidi kuwasimamia watumishi ili waweze kuwa na nyaraka hizo.
Kufuatia maelezo ya Afisa Utumishi ndipo Naibu Waziri akasema "Watumishi wote acheni kufanyakazi kwa mazoea , nyakati hizi si za kufanya kazi kwa mazoea". Pia alisisitiza kuwa katika ziara iatakayofuata atachukua hatua kali kwa watumishi wazembe na wasio na mipango kazi pamoja na OPRAS.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Wakiwa Nje ya Ukumbi wa Halmashauri Wakisikiliaza Hotuba na Maagizo ya Mhe. Deo Ndejembi Naibu Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.