Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, MH. JUMAA H. AWESO (MB) amefanya ziara Wilayani Mpwapwa mnamo tarehe 03.11.2017 ambapo alitembelea miradi mbali mbali ya Maji inayotekelezwa hapa Wilayani. Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Mradi wa maji wa Kimagai , mradi unaotekelezwa kupitia ufadhili wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji ( WSDP). Kijiji hiki kipo katika Kata ya Kimagai na kina jumla ya wakazi wapatao 3483 kwa kwa mujibu wa takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012. Mradi ulijengwa na Kampuni ya PATRIARCH Co. Ltd ya Arusha, chini ya usimamizi wa Mhandisi Mshauri Kampuni ya O & A Consult. Ltd ya Dar es Salaam. Gharama ya Mradi ni Tshs. 347,486,698.00 kwa Mkandarasi aliyejenga na Tshs. 34,401,183 za usimamizi, Kampuni ya O & A Consult. Ltd ya Dar es Salaam na kufanya jumla ya fedha zote zilizotumika kwenye mradi huu kuwa Tshs. 403,791,281.00. Mradi unasimamiwa na Chombo Huru cha Watumiaji Maji (COWSO) kilichoundwa na Halmashauri ya Wilaya kwa kushirikiana na Wananchi wa Kimagai. Hata hivyo kutokana na changamoto za Uendeshaji Kijiji kupitia Chombo Huru cha Watumiaji Maji, kimeingia Mkataba na Wakala kwa ajili ya kuendesha mradi Mafanikio baada ya mradi kukamilika 1. Zaidi ya asilimia 93% ya wananchi wa Kimagai wamefikiwa na huduma ya maji baada ya mradi kukamilika. 2. Hadi sasa kiasi cha fedha kilichopo benki ni Tshs. 2,600,000. 3. Wananchi wanapata huduma ya maji kwa karibu 4. Ujenzi wa nyumba bora umeongezeka. 5. Magonjwa ya milipuko yamepungua. 6. Mahudhurio shuleni yameongezeka. 7. Kupata mradi mwingine wa vyoo matundu 8 yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Kimagai.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.