(Na: Shaibu J. Masasi : Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (Mbunge) amefanya ziara ya siku moja wilayani Mpwapwa akiwa na timu ya mazingira toka Wizara ya Muungano na Mazingira. Katika ziara hiyo Mhe. Naibu waziri ameambatana na wataalamu toka NEMC (The National Environment Management Council), TFS (Tanzania Forest Services) pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Mhe. George Lubeleje, makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime, Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Mpwapwa Ndg. Maria Leshalu pamoja na wataalamu wengine toka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Katika ziara yake Mheshimiwa Naibu Waziri ametembelea na kujionea korongo kubwa lililokatiza kata ya Mpwapwa Mjini ambalo linaendelea kutanuka na kuleta maafa makubwa wakati wa mvua za masika. Kwa ujumla korongo hili limepanuka sana na linaendelea kutanuka kila mwaka kipindi cha mvua za masika. Kaimu Afisa Mazingira Wilaya Ndg. Theodory Mulokozi amemueleza Naibu waziri wa Wizara ya Muungano na Mazingira kuwa sababu zinazopelekea korongo hili kutanuka ni kutokana na uharibifu wa mazingira uliofanywa na watu wanaoishi kijiji cha Kiboriani achacho kipo juu ya mlima ambao korogo hili huanzia. Akiendelea kueleza Kaimu Afisa Mazingira amezitaja baadhi ya shughuli zilizofanywa na wakazi wa Kijiji cha Kiboriani na kusababisha korongo kupanuka ni pamoja na kulima katika miteremko ya milima kukata miti na ufugaji holera.
Naibu Waziri wa Wizara ya Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (wapili kushoto) na Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Mhe. George Lubeleje (wakwanza kushoto) wakikagua korongo kubwa lililopita Mpwapwa Mjini
Pia Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwaa amezitaja juhudi zilizofanywa na halmashauri katika kuthibiti kupanuka kwa korongo hilokuwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi wote kwa ujumla na hasa waishio katika kijiji cha kiboriani, kuwahamisha baadhi ya wanakijiji waliokuwa wamevamia eneo tengefu la hifadhi la korongo hilo na kushirikiana na TFS kuthibiti shughuli za uchomaji mkaa katika maeneo yote ya Wilaya ya Mpwapwa na hasa mlima kiboriani ambako ndio chanzo cha korongo hilo. Pia Halmashauri kwa kushrikiana na TFS imekuwa ikiwakamata waaribifu wa mazingira hasa wakataji miti na kuwafikisha katika vyombo vya sheria ambapo baadhi yao wameshahukumiwa na wengine kesi zao bado zipo mahakamani upelelezi haujakamilika. Vile vile Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imechukua tahadhari kwa kujenga ukuta wa zege (Gabions) katika maeneo yanayoendelea kupanuka na zile ambazo maji ya mvua za masika huchimba na katika maeneo muhimu kama vile katika madaraja na mwambao wa majengo ya wananchi na serikali.
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi ameelezea athari zinazotokana na kuwepo kwa korongo hilo kipindi cha mvua za masika ni kukatisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi kwa kuwa miundombinu ya barabara huharibiwa, baadhi ya wananchi na mali zao kusombwa na maji, nyumba kusombwa na mafuriko yanayaosababishwa na korongo hili na hivyo kupelekea vifo.
Ukuta wa Zege (Gabion) uliyojengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa katika Daraja la Vinghawe (Daraja ambalo linaunganisha Kata ya Vinghawe, Mpwapwa Mjini, Lupeta na Godegote)
Baada ya kujioneao na kukagua Naibu waziri wa Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima, kwanza amepongeza juhudi zote zilizofanywa na halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuendelea kulithibiti korongo hilo. Vile vile amehaidi kulithibiti korongo hili na kuzitatua changamoto zote za korongo hilo, hivyo kwa kuwa jitihada za haraka zinahitajika, Naibu Waziri amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Mpwapwa Ndg. Maria Leshalu kuwasilisha andiko rasmi la kuomba usaidizi wa kuthibiti korongo hili katika ofisi yake ili aweze kuchukua hatua za haraka iwezekanavyo.
Pia Mbunge wa jimbo la Mpwapwa Mhe. George Lubeleje amesema kuwa Baraza la Madiwani la Wilaya ya Mpwapwa limejadili na kuazimia mbinu mbalimbali za kukabiliana na uharibifu wa mziangira na amewaomba wanasiasa wenzake kuwa mstari wa mbele katika kukomesha uharibifu wa mazingira na kujadili agenda za uharibifu wa mazingira katika vikao vya kisheria na kuwahamasisha wananchi wawafichue waharibifu hao.
Naibu Waziri wa Wizara ya Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima (aliyesimama katikati mwenye suti nyeusi) akikagua uharibifu wa mzingira katika safu za milima ya Kiboriani kata ya Mazae Wilayani Mpwapwa
Hata hivyo Naibu Waziri ameitaka Wilaya ya Mpwapwa ianze kutenga maeneo kwa ajili ya wananchi kupata nishati ya kuni na mkaa, kutenga maeneo ya ufugaji na ya kilimo, hii itasaidia kuepuka migogoro ya maliasili miongoni mwa pande zinazonufaika. Pia amesema hii itaongeza uwajibikaji miongoni mwa wananchi kuweza kuyatunza maeneo yao vizuri ili waendelee kupata faidi zitokanazo na maendeo hayo.
Mwisho Naibu Waziri amevutiwa na mazingira ya Chuo cha Ualimu Mpwapwa na kusababisha kwenda kutembelea chuo hicho, hakina amejionea jinsi chuo kilivyopandwa miti na maua vizuri. Akielezea Makamu Mkuu wa Chuo hicho kuwa kwa sasa cho kimejiunga na program ya Kisiki Hai kwa maana chuo kitaendelea kupanda miti katika maeneo yasiyo na miti. Pia Naibu Waziri amezitaka taasisi zote ziliizopo wilayani Mpwapwa ziweze kuiga mfano huu wa Chuo cha Ualimu katika kutunza mazingira.
Chuo cha Ualimu Mpwapwa Kimepongenzwa na Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Kwa Utunzaji wa Mazingira
Kwa taarifa zaidi pakua nyaraka hii:
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.