(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mwenge wa Uhuru 2019 umeingia Wilaya ya Mpwapwa na kukembelea, Kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mitano yenye thamani ya Tsh. 711,733,640.89 Miradi hiyo ni Mradi wa Ufugaji nyuki uliopo kwa Mshango kata ya Vinghawe, mradi wa Wodi ya matibabu ya Utapiamlo mkali iliyopo katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa kata ya Mpwapwa Mjini yenye thamani ya Tsh 130,480,586.00, mradi wa Mnada wa kisasa wa Ilolo uliopo kata ya Mpwapwa Mjini, mradi wa Maji Mzase uliopo kata ya Berege na mradi wa Maktaba ya Shule ya Sekondari Kibakwe iliyopo kata ya Kibakwe.
Mwenye wa Uhuru 2019 unaoongozwa na Mkimbiza Mwenge Kitaifa Ndugu. Mzee Mkongea Ali amekubali kuweka jiwe la msingi katika jengo la wodi ya utapiamlo mkali japo kuna maelekezo ya marekebisho machache ameyatoka ili yafanyiwekazi kama kutenganisha chemba ya maji ya bafuni na kunawa mikoni yanatoka katika masinki ya kunawia.
Pia amekubali kutembelea mradi wa ufugaji nyuki na kugawa mizinga ya nyuki 28 kwa vikundi vya ufugaji nyuki kwa Mshango katika kata ya Vinghawe. "Nawagawai mizinga hii kweli mfanyekazi ya ufugaji nyuki na kutunza mazingira ya sehemu hii hasa upanda wa miti, uhifadhi wa vyanzo vya maji na kutochoma moto ovyo" amesema Ndugu. Ali.
Naye Waziri wa Nchi, ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. George Simbachawe amepata fursa ya kuongea na wananchi wa Mpwapwa juu ya utunzaji wa mazingira kwa kuwataka wananchi wa wilaya ya Mpwapwa kupanda miti maji, kutunza vyanzo vya maji, kutochoma moto misitu, kutochungia na kulima katika vyanzo vya maji na kufuga nyuki ili kujipatia kipato mmbadala. Pia amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri kusimamia zoezi la uwekwaji alama katika maeneo yatakayozuiawa wananchi kufanya shughuli za kibinadamu hasa katika vyanzo vya maji kwa sheria ya kutofanya shughuli za kibinadamu mita 60 toka katika chanzo.
Aidha Mwenge wa Uhuru 2019 umezindua Miundombinu ya Mnada wa Ilolo ambao ni mnada wa kisasa kwa wilaya ya Mpwapwa wenye mazizi mawili makubwa ya mbuzi na ng'ombe, machinjio ya kisasa, ofisi za wakusanya ushuru na wasimamizi wa mnada na pakilio la ng'ombe. Ndugu. Mzee Mkongea Ali amekubali kuzindua miundombinu hii japo ametoa maelekezo machache ya kuboresha ofisi za wasimamizi wa mnada kwa kuwa hazi madirisha ya vioo ili kuzuia vumbi na mvua kuweza kuingia.
Vile vile Mwenge wa Uhuru 2019 umetembelea Mradi wa maji Mzase ambao umekataliwa kuzinduliwa kwa kuwa upo chini ya kiwango kwa mujibu wa Mkimbiza Mwenge kitaifa Ndugu. Ali, amesema "Mradi huu wa maji haujakidhi vigezo kama nondo na matofali hakupelekwa maabara kupimwa, ulizio uliozungushiwa katika kisima na tanki la maji sio ulioonyeshwa katika BOQ" hivyo mradi huu hautazinduliwa na mwenge wa Uhuru 2019, amesisitiza. Badala yake ameruhusu wananchi kutomia maji hayo ni safi na salama kwa matumizi ya binadamu. Pia kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge 2019 kitaifa amemuogiza Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Mpwapwa Bi. Juliet Mtuyi kuchunguza mradi wa maji Mzase na taarifa ipelekwe TAKUKURU makao makuu na yeye apate nakala popote alipo.
Mwisho, Mwenge wa Uhuru 2019 umezindua maktaba ya kisasa katika shule ya sekondari Kibakwe japo ametoa maelekezo machache ikiwemo kuogeza viti, meza na vitabu ili wanafunzi waweze kupata fursa nzuri ya kujisomea.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.