Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge ametoa maagizo kadha Wilayani Mpwapwa katika kikao cha Baraza la Hoja lililofanyika leo tarehe 11 Julai 2018 ukumbi wa Mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Katika baraza hilo lililohudhuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa Mhe. George Lubeleje, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri, Waheshimiwa madiwani, Mkurugenzi Mtendaji, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Wakaguzi wa Nje, na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia kwa umakini baraza la hoja Wilayani Mpwapwa (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Aidha kwa ukagunzi uliofanyika mwaka 2016/2017 Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imepata Hati Safi ambapo Mkuu wa mkoa amepongeza sana kwa kupata hati hiyo ila ametoa tahadhari kwa uongozi wa wilaya ya Mpwapwa kutobweteka kwa hati hiyo na wanapaswa kufanyakazi kwa kufuata taratibu, sheria na kanuni ili kutozalisha hoja zingine.Ameongeza kuwa taratibu zikifuata halmashauri itakuwa haina hoja.
Aidha Mkuu wa Mkoa huyo amesifu kwa namna hoja zilifyojibiwa kwa kubanga hoja, mapendekezo ya mkaguzi, majibu ya menejimenti, mapendekezo ya kamati ya fedha, uongozi na mipango pamoja na mapendekezo ya baraza la hoja.
Pia Mkuu wa Mkoa ametoa ushauri kwa uongozi wa wilaya ya Mpwapwa kuwa ipange ratiba ya kusikiliza Migogoro yote ya ardhi, kupatiwa ufumbuzi, na kutunza kumbukumbu ya migogoro hiyo, 20% ya vijiji ipelekwe vijijini ikafanye maendeleo ngazi ya vijiji, 10% ya wanawake na vijana pia ipelekwe kwa walengwa na wahamasishwe kuunda vikundi vyenye tija ili waweze kutumia fedha hizo katika kuleta maendeleo na sio kutumia kwa matumizi binafsi.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia kwa umakini baraza la hoja Wilayani Mpwapwa (Picha Na. Shaibu J. Masasi - Afisa TEHAMA , Mpwapwa)
Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa Ametoa maagizo yafuatayo kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa:-
1. Kukusanya mapato kwa kutumia Mashine za Kielektroniki (POS) na kuwachulia hatua kali watu wote wanaohujumu mapato kupitia POS.
2. Kutohamisha fedha za mradi mmoja na kwenda kwenye mradi mwingine.
3.Kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuvisimamia kimamilifu ili kuongeza Mapato ya kutosha.
4. Kuboresha miundombinu ya shule kama vile madarasa.
5. Viongozi wa Vijiji na mitaa waitishe vikao vya kisheria na wasome mapato na matumizi.
6. Kuanza kufanya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Disemba 2019.
7. Viongozi waamasishe wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuupokea mwenge wa uhuru unaotarajiwa kupokelewa kimkoa wilayani Mpwapwa
tarehe 30 Julai 2018 na kuzindua miradi 6.
8. Kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya makazi na biashara.
9. Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kuhakikisha Wilaya ya Mpwapwa inakuwa salama hasa ukizingatia sasa Dodoma ni Jiji na tunapata wageni wengi
toka maeneo mbalimbali na nchi jirani.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.