(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mradi wa TIMIZA MALENGO umetoa Mafunzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa maafisa Kilimo na mifumo toka ngazi za kata na vijiji ambapo mafunzo haya yamefanyika katika Ukumbi wa Mamlaka ya Maji Wilayani Mpwapwa. Mafunzo haya yameanza leo tarehe 24/09/2019 hadi 28/09/2019, kwa muda wa siku tano.
Dhumuni la mradi huu ni kutoa mafuzo ya ujasiriamali kwa wasichana balehe na wanawake vijana kutoka katika kaya zinazotekeleza Mradi wa TASAF. Mafunzo haya yanafadhiriwa na TAYOA na TACAIDS. Wawezeshaji wa mafunzo haya toka ngazi ya Taifa ambao wametoa mafunzo haya ni pamoja na Ndug. Halima Mila na Ndug. Amour. Baada ya mafunzo haya, washiriki wataenda kuwafundisha wasichana balehe na wanawake vijana katika ngazi ya vijiji na watafundisha kwa muda wa siku 12.
Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa (katikati) akiwa katika picha za pamoja na wawezeshaji wa Kitaifa wa Mradi wa TIMIZA MALENGO
Mafunzo yatahusisha kuandaa mipango ya biashara itakayolenga kujiongezea kipato na kuibua shughuli za kiuchumi, na namna ya kutekeleza mipango kazi hiyo. Katika mafunzo haya kuna wawakirishi watano toka Halmashuri ambao watakuwa wasimamizi wakuu wa mradi na kutoa taarifa mbalimbali za mradi ili kufanikisha mradi huu.
Nae, Mkuregenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Paul Mamba Sweya amewasisitizia washiki kuwa wasikivu na kuuliza wanaoona hajaelewa ili kwenda kutekeleza mradi huu mzuri wenye nia ya kuwakwamua vijina hususani wanawake. Pia ameahidi kutoa ushirikiano kwa lolote litakalohitajika ili kutekeleza mradi huu.
Pia washiriki wameshukuru ujio wa mradi huu na fursa zake kwa kuwa utawajengea wao na walengwa elimu ya kutosha ya kuanzisha na kusimamia shughuliz za kiuchumi.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.