Wadau Mradi wa Lishe Endelevu unaofadhiriwa na Shirika la Deloitte wamepata fursa ya yapitia Maazimio ya Kamati ya Lishe ya Wilaya ya Mpwapwa katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Wadau waliohudhuria ni pamoja na wajumbe wa kamati ya lishe ya wilaya, Deloitte, na wataalam wa lishe toka mkoa wa Dodoma.
Katika kikao hicho wadau toka Deloitte wanaotekeleza mradi wa Lishe endelevu wahusia pia na kuwadhili watoto chini ya miaka mitano, vijana barehe na wanawake waliookatika umri wa kuzaa.
Madhumuni ya kikao hicho ni kukaa na kamati ya lishe ya Wilaya kuona na kupitia maazimio yaliyowekwa mwezi Aprili 2019 je, yametekelezwa kwa kiwango gani. Pia kuangalia changamoto zinazoikabili kamati ya Lishe ya Wilaya ya Mpwapwa.
Vilevile wadau mbalimbali wanaoshirikiana moja kwa moja na kamati ya lishe ya wilaya waliorodheshwa ili kutambulika kwa wadau wa Deloitte, wadau hao waliotambuliwa ni kama vile:- Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Jukwaa la Vijana wa Kitanzania (TAYOA), Mradi wa Kupambana na Malaria kwa watoto chini ya Umri wa Miaka mitano (PSI), Mfuko wa Kuboresha Afya (EGPAF), Plan International, Shirika la Chakula Duniani (FAO), na Kituo cha Matibabu cha Katoliki Dodoma (DCMC).
Changamoto zinazoikumba kamati ya lishe ya wilaya ni kama uelewa mdogo wa jamii juu ya lishe bora kwa watoto ambapo elimu inaendelea kutolewa na ukosefu wa fedha katika kutekeleza shughuli za lishe kimamilifu.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.