Mradi wa Stadi za maisha Compaign For Femel Education(CAMFED) umewafikia wana Mpwapwa na kuweza kutoa semina kwa Maaafisa Elimu kata,Wakuu wa Shule na Walimu walezi,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi.Mwanahamisi H.Ally amefungua mafunzo hayo Mei 14,2024 katika ukumbi wa HalmashauriBi Mwanahamisi ametoa rai kwa washiriki wa mafunzo hayo kuchukua jukumu la kuhakikisha mafanikio ya mradi na kujikita katika kuumiliki kwa dhati,na kuasisitiza kufanyakazi kwa bidii ili kuhakikisha vijana wanapata ujuzi wa stadi za maisha wanazohitaji kujikwamua katika lindi la maadili yasiyofaa.
Pia amesema faida za mradi ni kutambua stadi za maisha na si elimu ya darasani bali ni kuhusu kujitambua kwa vijana na maisha ya baadae kwa kuzingatia mipango na malengo iliyoratibiwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaaa (TAMISEMI)na CAMFED na kuwa imani na jamii yetu kuweza kubadilika kwa kasi
Vileviele amesema mradi una fursa nyingi za kuimaisha ujuzi wa vijana wetu kwa kuitambua na kujishuhulisha na shuhuli mbalimbali za ujasiria mali na uongozi pamoja na kujenga misingi imara ya Taifa endelevu na kupitia mafunzo hayo vijana watapata kujiamini kufikia malengo yao.
Mwisho amewasihi wana warsha kutoa Ushirikiano ili kufanikisha mradi,ili kuweza kuleta mabadiliko chanja ya vijana wetu na kushirikiana kwa pamjaa na CAMFED tunaweza kuchochea maendeleo ya jamii yetu kupitia vijana wenye stadi za maisha.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.