Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amekabidhi vitambulisho 3,500 vya wajasiliamali vya awamu ya pili kwa Maafisa Tarafa. Kwa sasa Mkuu wa Wilaya amebadili mfumo wa ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa kuwagawia Maafisa Tarafa ili wao wakawagawie watendaji wa kata na kusimamia ugawaji wa vitambulisho hivyo. Pia watendaji wa kata kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji watawagawia wajasiliamali walioandikishwa na wenyesifa zilizoainishwa.
Mkuu wa Willaya ya Mpwapwa (kulia) akimkabidhi Afisa Tarafa wa Mpwapwa Gloria Balegu (kushoto) vitambulisho vya wajasiliamali.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa ameamua kubadili mfumo wa kugawa vitambulisho baada ya mbinu ya kwanza ya kutumia kamati maalam ya kugawa vitambulisho iliyozunguka Wilaya nzima kushindwa kutoa mafanikio mazuri kwa kuwa baadhi ya vitambulisho vimebaki na vilivyogawiwa kwa wajasiliamali ni vitambulisho 238 mpaka sasa.
Leo Mkuu wa Wilaya ametoa maelekezo kwa Maafisa Tarafa 4 na watendaji wa kata 33 ili kuwapa mikakati sahihi ya jinsi ya kugawa vitambulish vya wajasiliamali na kuvimaliza. Kwa upande wao Maafisa Tarafa na watendaji wa kata wamekubali kufanya kazi hiii kwa umakini mkubwa na wamehaidi kuwa watakuwa wanatoa taarifa kila wiki ya jinsi zoezi hili linavyokwenda.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa (kulia) akimkabidhi Afisa Tarafa wa Rudi (kushoto) vitambulisho vya wajasiliamali.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.