(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imetajwa kuwa ni moja wapo ya Halmashauri inayofanya vizuri katika mambo mbalimbali kama vile Utawala, usimamizi wa miradi na Ukusanyaji wa Mapato. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Msaidizi Menejimenti ya Serikali za Mitaa Ndugu. Emmanuel Kuboja katika Kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa tarehe 06/03/2019.
Katibu Tawala Masaidizi menejimenti ya serikali za Mitaa Ndug. Emmanuel Kuboja (wa kwanza kushoto aliyesimama), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Paul Mamba Sweya (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Donath S. Nghwenzi (wa pili kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime (wa kwanza kulia) wakiwa katika Kikao cha Baraza la Madiwani.
"Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma ina imani kubwa na uongozi wa sasa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kuwa mapato kwa sasa yameimarika na kwa takwimu nilizonazo mpaka sasa mmekusanya mapato ya ndani kwa asilimia 74.26 " amesema Ndugu. Kuboja. Pia amemshukuru Mwenyekiti wa Halmasahuri ya Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Donath S. Nghwezi kwa kuendesha baraza la madiwani kwa umairi mkubwa. Vile vile Ndugu Kuboja ameeleza kuwa Mpwapwa inaweza kuwa Mamlaka ya Mji au Manispaa moja kwa moja kama ukusanyaji wa mapato na mikakati mizuri mliyoweka itaendelea hivi hivi.
Ndugu Kuboja ameongeza kuwa katika bajeti ya mwaka huu 2019/2020 mnatakiwa kuzingatia vipaumbele vya Kitaifa, Kimkoa na Kiwilaya, kwanza; kuweka juhudi katika Elimu hasa katika kujenga madarasa na kuongeza juhudi ili kuhakikisha ufaulu unaongezeka. pili, kuweka mikakati kuhamasisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuwa wafadhiri na fedha toka Serikali Kuu zimepunguzwa. Pia ameongeza kama kuna mtu atakaye haribu utaratibu huu mzuri mlioweka wa kukusanya napato hatua kali zikuliwe dhidi yake.
Waheshimiwa madiwani, wakuu wa idara na wageni waalikwa wakiwa katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amewaeleza Waheshimiwa Madiwani kuwa kwa sasa mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa yameongeza na kasi ya ukusanyaji wa mapato imeimarika, kwa taarifa iliyopo mpaka mwisho wa mwezi huu wa Februari mapato yamekusanywa na kufikia asilimia 85 ambayo bado hayajatumwa katika mfumo ndio maana katika mfumo bado kuna taarifa ya asilimia 74.26. Mwaka jana 2018 mwezi kama huu kulikuw na asilimia 26 tu ya makusanyo ya mapato ya ndani ndio maana tulichukua hatua zile na nyote mlishuhudia , amesema Mhe. Shekimweri. Kwa sasa inaonyesha kuwa kuna jitihada zinafanyika katika kukusanya mapato.
Pia Mhe. Kimweri amewataka wataalam na waheshimiwa madiwani kufuata sheria, kanuni na taratibu katika kufanya kazi za umma. "Wito wangu kila mmoja wenu afuate Sheria, Kanuni na Taratibu, mashinikizo yoyote hayatawaweka salama".
Mwisho Mkuu wa Wilaya amemtaka Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu Pius Sayayi kuwaelekeza watumishi sheria, kanuni na taratibu kupitia baraza la watumishi na hasa watumishi wapya.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.