Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa Dc
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ipo katika Mpango wa Uuzaji wa Viwanja 1289 katika Eneo la Mazae Block "E". Eneo hilo lipo katika kata ya Mazae na viwanja vipo umbali wa mita 50 kutoka barabara kuu ya Mpwapwa - Dodoma. Katika viwanja hivyo kuna viwanja vya makazi, biashara, makazi na biashara, vyenye ukubwa kuanzia Mdogo, Kati na Kubwa zaidi. Viwanja hivyo vimepipwa na kupangiliwa kwa ustadi mkubwa ambapo kuna maeneo ya wazi, maeneo ya kukusanyia taka, maegesho, viwanja vya michezo, bustani, maeneo ya kujenga shule, nyumba za ibada na taasisi mbalimbali.
Linatokea Gari ndogo (kushoto) ni barabara ya kuingia eneo la Mazae Block "E" kutoka barabara kuu ya Mpwapwa - Dodoma
Kwa sasa Halmashauri ipo katika hatua ya kusafisha eneo hilo lenye jumla ya viwanja 1289 kwa kuchonga barabara kuu na za mitaa ambapo zoezi hilo kwa kiasi kikubwa limekamilika. Pia miundombinu ya maji na umeme itapatikana katika eneo hilo ambapo wataalam wa umeme toka katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wataalam wa Maji toka Mamlaka ya Maji Mijini na Vijijini (RUWASA) wa hapa Wilayani Mpwapwa wameshaanza kazi ya kukagua eneo la mradi na kutaka kuanza kazi mara moja.
Ramani ya Eneo la Mazae Block "E"
Akizungumza mbele ya Wakuu wa Idara waliotembelea eneo litakalojengwa Kituo cha Mabasi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Paul Sweya amesema "Zoezi la utengenezaji wa barabara limeshakamilika, sasa zoezi linalofuata ni kuweka miundombinu ya maji na umeme katika eneo la Mazae Block "E" linalotarajiwa kuuzwa viwanja 1289 hivi karibuni'. Ndugu. Sweya ameongeza kuwa "nawakaribisha wananchi kutoka maeneo yote ya Tanzania kuja kununua viwanja hivi ambavyo vipo Mkoa wa Dodoma na Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi hivyo, waje wanunue viwanja vilivyopo katika Makao makuu ya Nchi".
Kwa hiyo wananchi wote wenye nia na uwezo wa kununua viwanja hivyo wawe tayari muda wowote viwanja hivyo vitaanza kutangazwa kwa ajili ya kuuzwa.
******Mwisho******
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.