Wilaya ya Mpwapwa imepata Mkuu wa Wilaya Mpya Mhe. Josephat Paul Maganga awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ameteuliwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa baada ya Mkuu wa Wilaya wa zamani Mhe. Jabir Mussa Shekimweri kuteuliwakuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.Mkuu wa Wilaya Mpya (kushoto) akitambulishwa kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama nje ya Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa
Aidha makabidhiano ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa yamefanyika leo kati ya Mhe. Shekimweri na Mhe. Maganga katika Ofisi ya Wilaya ya Mpwapwa na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa Mhe. George Fuime ambaye pia ni diwani wa kata ya Mpwapwa Mjini, Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Paul M. Sweya, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa Ndugu. Sarah Komba, Wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama, Watumishi wa Ofisi ya mkuu wa Wilaya pamoja na baadhi y Wakuu wa Idarawa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Pia katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya wa zamani Mhe. Shekimweri kwanza amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma; Kisha ameeleza kwa kifupi masuala muhimu yaliyomo katika taarifa ya makabidhiano ya ofisi hususan amejikita kwenye changamoto mbalimbali na jitihada zilizofanywa na ofisi yake kabla ya kupata utezi wa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma. Changamoto hizo ni pamoja na;- Kukijanisha Dodoma ambapo Wilaya ya Mpwapwa imechagua zao la miti la korosho kuwa zao linaloweza kukijanisha Dodoma na kuleta tija baadae, Migogoro ya ardhi, uharibifu wa mazingira, Miradi hasa Ukumbi wa Halmashauri na Vituo vya Afya, Ujenzi wa Shule za Sekondari za kata kwa kata zisizo na sekondari, Madeni ya wakandalasi na watumishi, Maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Ujenzi ya Reli ya Kisasa ya Treni iendayo kasi (SGR) na ukarabati wa reli ya zamani, Ukarabati wa Chuo cha Ualimu Mpwapwa, na Maandalizi ya Mwenge wa Uhuru Julai 31, 2021.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya Mpya Mhe. Maganga ameahidi kuyatekeleza yale yote yaliyoanzishwa na mtangulizi wake kwa kuwa masuala yote ni muhimu na yamegusa kila nyanya za msingi.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.