(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imefanikiwa kujibu hoja zote za Mwaka wa Fedha 2017/2018 kwa usahihi na kuwarithisha wakaguzi wa nje na kupelekea kufunga asilimia 90 za hoja zote. Hayo yamesemwa na Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Emmanuel Abraham katika kikao cha Baraza la Hoja lililofanyika katika
Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa akiwa anawasilisha taarifa yenye hoja ya ukaguza kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.
Katika baraza hilo limejumuisha Waheshimiwa madiwani wa Kamati ya Fedha, Wakuu wa Idara na Wakaguzi wa Nje ambapo hoja zote zilisomwa, hoja hizo ni zile zilizfungwa,
zinazosubiri vielelezo toka kwa menejimenti na zilie zinazo subiri mabadiliko ya kitabia katika utendaji wa kazi wa kila siku. Katika baraza hilo imeelezwa kuwa jumla za hojanyingi za mwaka wa Fedha 2017/2018 zimefungwa na baadhi ya hoja zinasubiri uthibisho wa vielelez toka kwa menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Sambamba na kujibu hoja hizo kwa ukamilifu; Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ametangaza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imepata
Hati Safi kwa ukaguzi uliofanyika kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.
Wakaguzi wa Nje pamoja na Mshauri wa Fedha wa Mkoa wa Dodoma wamesifu jinsi hoja za mwaka wa Fedha 2017/2018 zilivyojibiwa kwa usahihi na kupelekea kupata Hati Safi.
Aidha Mkaguzi wa Nje Kanda ya Dodoma Bw. Njeleja Sasamka Chambi, ameishauri menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ikae na kufanyia kazi kwa haraka katika maeneo yenye mapungufu katika Ukaguzi.
Pia ameipokeza kamati ya Fedha pamoja na Menejimenti kwa kujibu hoja kikamilifu na hatimae kupelekea Hoja hizo kufungwa. Kwa zile hoja zinazohitaji vielelezo ili Hoja zifungwe menejimenti inaombwa kuwasilisha vielelezo hivyo mapema iwezekanavyo ili wakaguzi wajiridhishe ili kufunga hoja.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Paul M. Sweya amekubaliana na ushauri wa Wakaguzi wa Nje kuwa atashirikiana
na menejimenti yake ili kuwasilisha vielelezo mapema kwa wakaguzi wa nje ili kufunga hoja zilizobaki.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ambaye ni diwani wa Kata ya Mpwapwa Mjini Mhe. George Fuime amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kufanya haraka iwezekanavyo kupeleka vielelezo kwa wakaguzi wa nje kwa ajili ya uhakiki ili kufunga Hoja zote zilizobaki.
Mwisho amewaomba wakaguzi wa nje kushirikiana na Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kuwaelekeza mapungufu yote yaliyopo katika Hoja ili kutafuta
vielelezo vyake.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.