Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ni miongoni mwa Halmashauri 41 iliobahatika kufikiwa na mradi wa Uboreshaji Usalama na Umiliki wa Ardhi.Ndugu Paulo Kiteso mratibu wa mradi amesema lengo la mradi ni KUPANGA,KUPIMA NA KUMILIKI ardhi kisheria.
"Mradi utajenga na kukarabati ofisi,kupanga na kupima viwanja vya vijiji na maeneo"kiteso amesema
Vilevile ameelezea faida zitakazo patikana katika mradi ni kuweza kuondoa migogor ya ardhi,kutenga maeneo ya njia za miguu na maeneo ya huduma nyengine kama viwanja vya michezo,masoko na pia kutengeneza wigo wa ukusanyaji kodi katika maeneo ya kibiashara
Naye Meneja wa Majengo ya mradi Ndugu Awadh Salim amesema kwa upande wa Halmashauri,Kitaifa kila Mkoa utajenga jengo moja la ghorofa 1 na Mkoa itajenga ofisi za ardhi za Wilaya na vijiji.Mnamo tarehe 25.2.2024 mradi ulianza kusaini mkataba ambapo ikifika mwezi wa 5na 6 uzabuni wa mradi utaanza na ifikapo mwezi wa 8 mradi wa ujenzi utaanza.
Halmashauri 41 zitaguswa na mradi huu ambapo Halmashauri 23 zitajengewa majengo mapya,Halmashauri 11 zitafanyiwa ukarabati na Halmashauri 7 ambazo zina majengo mapya zitaboreshewa mfumo wa tehama,pia zitaboresha Taasisi za Elimu za vyuo vya Ardhi.Kwa upande wa jamii mradi utanufaisha wanajamii kwa kupata nguvu kazi itakayotokea eneo husika.
Kikao cha utambulisho wa Mradi kimefanyika April 15,2024 katika Ukumbi wa Halmashauri.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.