Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa hufanyika kila mwaka tarehe 25 Julai kama moja wapo ya kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa waliojitolea kwa moyo wa uzalendo kupigana vita vya ukombozi ili kuikomboa Nchi ya Tanzania katika mikono mwa wakoloni na watu wenye hira na tamaa ya kutaka kuitawala kimabavu.
Kwa mwaka huu wa 2018 siku hii ya mashujaa imeazimishwa kiwilaya hapa Mpwapwa kwa kufanya usafi katika maeneo muhimu ikiwemo Soko Kuu la Mjini Mpwapwa na Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa ambapo wananchi kwa ujumla wamejitokeza kwa wingi ili kushsiriki katika usafi huo. Pia baada ya zoezi la usafi kukamilika katika maeneo yote ilifuatiawa na zoezi la UCHANGIAJI DAMU kwa hiari, ambapo wadau walijitokea kufanikisha hili.
Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri, Wanajeshi wa JKT toka Kikosi cha Mpwapwa, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Waheshimiwa Madiwani, Wafanyakazi wa Umma na wananchi wamejumuika kwa pamoja na kufanya shughuli zote za usafi katika maeneo yote yaliyopangwa.
Kwa ujumla muitikio ulikuwa ni mzuri na hivyo usafi ulifanyika ipasavyo na kufanya maeneo yote kuwa safi.
Katika hotuba yake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa amewataka wananchi na wadau wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kama ilivyo katika siku hii ya leo katika siku ya usafi ya Jumamosi ya tarehe 28 Julai 2018 ili usafi uimalike. Pia ameongeza kuwa usafi uwe ni utamaduni wetu ambapo kila siku tufanye usafi katika maeneo yetu ya kazi pamoja na makazi.
Mhe. Jabir Shekimweri Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa (kulia) na Mhe. George Fuime Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa (kushoto) wakifanya usafi katika eneo la Hospitali ya Mpwapwa katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa tarehe 25 Julai 2018. (Picha. Na. Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa pamoja na wananchi wakifanya usafi katika eneo la mnara wa mashujaa katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa tarehe 25 Julai 2018.
(Picha. Na. Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Wanajeshi wa JKT kikosi cha Mpwapwa pamoja na wananchi wakifanya usafi katika eneo la kuzunguka Soko Kuu la Mpwapwa Mjini katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa tarehe 25 Julai 2018.
(Picha. Na. Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mhe. Jabir Shekimweri Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa akichangia damu kwa hiari katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa mara baada ya kumaliza zoezi la Usafi katika Siku ya Mashujaa tarehe 25 Julai 2018.
(Picha. Na. Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Baadhi ya Wanajeshi wa JKT wakiwa katika foleni ya uchangiaji damu kwa hiari katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa mara baada ya kumaliza zoezi la Usafi katika Siku ya Mashujaa tarehe 25 Julai 2018.
(Picha. Na. Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya Mpwapwa Afande Mafuru (wa kwanza kulia) na wanajeshi wa JKT kikosi cha Mpwapwa wakifanya usafi katika eneo la kuzunguka Soko Kuu la Mpwapwa Mjini katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa tarehe 25 Julai 2018. (Picha. Na. Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Kamanda Karuma wa jeshi la JKT Wilaya ya Mpwapwa akichangia damu kwa hiari katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa mara baada ya kumaliza zoezi la Usafi katika Siku ya Mashujaa tarehe 25 Julai 2018 (Picha. Na. Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.