KITUO cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kimeendesha Mafunzo kwa Mkurugenzi Mtendaji Bi.Mwanahamisi H Ally pamoja na Wakuu wa Idara na vitengo,mafunzo hayo yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo kuhusu majukumu ya PPPC yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Febuari 11,2025.
Mbia ni yule anaetekeleza majukumu yake kwa niaba ya Serikali,na baada ya kumaliza kwa mkataba wa mradi,mradi unarudi Serikalini.Mkataba wa mradi huo ni wa muda maalum kuanzia miaka mitano hadi thelathini.
Katika mambo ambayo yamejadiliwa ni pamoja umuhimu wa kutumia PPP ni kuhakikisha shuhuli za Ubia zinafanyika na kutekelezeka hususani kwenye Miradi ya kimaendeleo na huduma za kijamii.
Lengo kuu la Miradi ya Ubia ni kuwezesha Halmashauri kuweza kukidhi mahitaji wa rasilimali fedha kwa 90%
Kabla ya kuanzishwa kwa PPPC ilikuwa ni idara katika idara ya Fedha na baadae kufanyiwa maboresho ya Kisheria mwaka elfu mbili na ishirini.
Ofisi ya Kituo cha Ubia imeanza kazi rasmi mwaka elfu mbili na ishirini na nne.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.