Wadau wa kitengo cha Ustawi wa Wanyama Inades Formation ambao ni Taasisi inayojishuhulisha na ustawi wa wanyama hususani Punda leo Agosti 18,2025 wamefanya kikao na baadhi ya wakuu wa idara ambao watahusika na uendeshaji wa kimkakati na utetezi wa Mnyama kazi Punda katika ofisi za Kilimo Mpwapwa.
Katika tafiti zao walizozifanya wakishirikiana na Taliri wamebaini kuwa mnyama kazi Punda anafaida nyingi sana katika jamii,lakini pia jamii hiyo humtumia vibaya na kumfanyia ukatili mkubwa ndani yake ikiwemo kuchinjwa na kubebeshwa mizigo mizito inayompelekea kuchunika kwa ngozi yake kutokana na msuguano wa kamba.
Inades formation ina lengo la kuweza kumtunza mnyama kazi Punda na kuweza kufanya nae kazi vizuri,kwa upande wa Mpwapwa Vijiji viwili vimebahatika kupata mradi huu ambavyo ni Kingiti na Gulwe kwa kusaidiwa kuanzisha vikundi mbali mbali kama vya ujasiria mali na ufugaji wa mbuzi na kuku kupitia vikundi vya ufugaji na watumiaji wa Punda na pia wanafanya shuhuli za kujiwekea hakiba na kuanzisha mashamba ya malisho kwa ajili ya wanyama wao.
Kwa upande wa Shule wametoa elimu inayohusiana na usawi wa wanyama hususani mnyama kazi Punda,utunzaji wa mazingira na kuandaliw kuwa mabalozi bora kwa wenzao ambapo jumla ya shule 12 walipatiwa elimu hiyo.
Mradi huu wa kumlinda mnyama kazi punda unamkakati wa uanzilishwaji wa jukwaa la kimaendeleo ambalo litatumika kujitegemea na kujiendesha ili kuweza kusonga mbele kimaendeleo na pia kwenye ngazi za Shule iweze kutumika mchoro ambao utamlinda mnyama kazi Punda.
Mradi wa kumtunza mnyama kazi Punda unafanyika Mikoa mitatu,Dodoma,Iringa na Singida,kwa upande wa Dodoma unafanyika Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa na jumla ya vikundi ji 893,vijiji 12 na vikundi vya watumiaji na wafuga Punda ni 45 na jumla ya Punda 1164 wapo ndani ya bikundi hivyo.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.