Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mh. Jabir Shekimweri akishirikiana na watumishi pamoja na wananchi katika Jumamosi ya Usafi wa Mazingira. Katika shughuli hiyo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya afanya usafi katika Soko la Mji Mpya lililopo Kijiji cha Ilolo kata ya Mpwapwa mjini katika Wilaya ya Mpwapwa. Pia mwitikio wa wananchi na watumishi katka zoezi hilo likuwa mzuri kiasi kwamba usafi ulifanywa katika katika eneo lote la soko hilo.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa (Kulia pichani) akifanya usafi wa mazingira katika Soko la Mji Mpya.
Watumishi na Wananchi wa Wilaya ya Mpwapwa wakifanya usafi wa mazingira katika Soko la Mji Mpya.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.