Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mh. Jabir Shekimweri ameitisha kikao cha dharura kujadili usafi wa mazingira kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha ambazo zinasababisha kusomba na kusambaza takataka ovyo katika Mji wa Mpwapwa. Kikao hicho kimehudhuriwa na wataalam mbalimbali wakiwemo Elimu, Afya, Ardhi, Kilimo, Mifugo na Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Mkuu wa Wilaya katika kikao hiki amezungumnzia mambo yafuatayo:-
1. Usafi wa Mazingira
Aidha Mkuu wa Wilaya amesisitiza wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha anafanya usafi katika makazi yake, kutumia vyoo vizuri ili kuepuka magonjwa ya kipindupinu, kufanya usafi katika mitaro na miundombinu ya maji au vyanzo vya maji. Pia amesisitizia kuwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi baada ya usafi atakuwa anafanya kikao kidogo na wanaichi ili kuwahimiza kuwa na mazoea ya kufanya usafi. Vilevile amasema kuwa sheria ziko wazi kuhusu uchafunzi wa mazingira hivyo atakayechafua mazingira hasa kutupa taka katika korongo linalopita katikati ya mji wa Mpwapwa anaweza kutozwa faini ya kuanzia Tsh. 50,000/- hadi Tsh. 500,000/-
2. Ulinzi na Usalama
Mkuu wa Wilaya ameitaka kamati ya Ulinzi na usalama pamoja na wananchi wote kwa ujumla kuhakikisha wanawazuia watoto wanaocheza kwenye madibwi na mito katika kipindi hichi cha mvua. Pia ameongeza kuwa uchimbaji kiholela wa madini ya ujenzi katika kipindi hiki cha mvua si vizuri kwa kuwa kunasababisha mmomonyoko wa udongo na matibwi makubwa.
3. Kilimo
Katika Kilimo Mh. Shekimweri amesema, wananchi wanapaswa kulima kipindi hichi cha msimu wa mvua na kujiwekea mikakati ya kuondoa njaa kwa kulima mazao kama Mtema, mihogo, na mahindi. Pia amesema lianzishwe daftari maalum la kurekodi wakulima na Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika afuatilie kwa karibu ili kutoa msaada wa kilimo unapohitajika.
4.Elimu
Idara ya Elimu ihakikishe miundombinu kama madarasa na vyoo inakuwa salama ili wanafunzi wapatiwe elimu wakiwa mahali pa usalama. Pia amesema, wanafunzi wapewe elimu juu ya madhara ya kupata,kumpa mwanafunzi mwenzie, na kutoa mimba.
5. Afya
Katika kuhakikisha huduma ya Afya inamfikia kila mwananchi anapohitaji, Mkuu wa Wilaya amewata wananchi wa Mpwapwa kuwa na bima ya Afya amabayo itamuwezesha kupata huduma ya matibabu hata kama atakuwa hana pesa kwa wakati huo.
Wataalam mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya.
Wataalam mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya.
Hitimisho:
Mkuu wa Wilaya amesisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma waliopewa dhamana ya kusimamia masuala mbalimbali katika jamii wafanye hivyo. Pia amewaonya watumishi hao kuwa wasipowajibika ipasavyo watawajibishwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.