(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amefanya ziara katika shule ya Sekondari Kibakwe kukagua maendeleao ya ujenzi wa madarasa matatu kwa ajili ya kuwapokea kidato cha kwanza tarehe 7 Januari 2019. Akiwa katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya amejionea jinsi ujenzi unavyoendelea katika shule hiyo ambapo kwa sasa ujenzi wa madarasa hayo yapo katika hatua ya kuweka jamvi.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri (katikati) akitoa maelekezo katika eneo linalojengwa mdarasa katika shule ya Sekondari Kibakwe, (wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Paul Mamba Sweya)
Mkuu wa Wilaya hakuridhishwa na kasi ya ujenzi huo wa madarasa, hivyo amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Paul Mamba Sweya kuwa ahakikishe ujenzi huo unaenda kwa kasi na mafundi wanasimimiwa kwa ukaribu sana.
Haiwezekani na haikubaliki mpaka leo ujenzi wa darasa uwe katika hatua ya msingi wakati tarehe 7 Januari 2019 wanafunzi wa kidato cha kwanza wataanza kuja kuripoti, tutawaweka wapi? amehoji Mhe. Shekimweri.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Shekimweri ametoa agizo kwa kamati ya ujenzi kusimamia kazi ya ujenzi masaa 24 na ametoa siku 14 madarasa yakamilike kuanzia leo. Pia Mkuu wa Wilaya amehadi kuanzia tarehe 3 Januari hadai 4 Januari 2019 ataenda katika eneo la ujenzi wa madara yao kusimamia usiku na mchana kwa hiyo atalala katika eneo hilo ili kuhakikisha kuwa mafundi wanakamilisha kwa wakati.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Paul Mamba Sweya (wa kwanza
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.