Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri, leo tarehe 23 Mei 2018 atembelea na kukagua Miradi yote ya Wilaya ya Mpwapwa inayotarajiwa kutembelewa na Mwenge wa Uhuru tarehe 30 Julai 2018. Katika kutembela na kukagua miradi hiyo Mkuu wa Wilaya ameambatana na kamati ya mwenge ya wilaya ili kubaini mapungufu na kuagiza kuyafanyia marekebisho.
Ikumbukwe kuwa Mkoa wa Dodoma mnamo tarehe 30 Julai 2018 unatarajia kuupokea Mwenye wa Uhuru kimkoa katika Wilaya ya Mpwapwa kata ya Lumuma ukitokea Mkoa wa Morogoro wilaya ya Kilosa. Katika mapokezi ya mwenge huo wanatarajiwa kuhudhuria wakuu wa mikoa wote wawili wa Mkoa wa Morogoro na Dodoma, wakuu wa Wilaya zote za Morogoro na Dodoma, Wakurugenzi wote wa Morogoro na Dodoma, makatibu tawala wa wilaya zote Morogoro na Dodoma, na wageni wengine waalikwa katika sherehe hizi, pamoja na wananchi wote kwa ujumla.
Kwa upande wa Wilaya ya Mpwapwa Mwenge huo unatarajiwa kutembelea miradi ifuatayo: Shule ya Awali na Msingi ya Franco Badian iliyopo kata Lumuma, Kituo cha Afya cha Pwaga kilichopo kata ya Pwaga, Kituo cha Wanyama kazi Kibakwe kilichopo kata ya Kibakwe, Barabara ya Kidenge - Lufu, Mradi wa Maji wa Luhundwa, The Mother land shule ya English Medium iliyopo kata ya Mpwapwa Mjini katika Kijiji cha Ilolo na Kiwanda cha Kukamua alizeti, kusaga na kudindika unga wa mahindi. Hivyo miradi hiyo yote imetembelewa na kukaguliwa na mkuu wa wilaya na timu yake ya kamati ya ulinzi na usalama.
Shule ya Awali na Msingi ya Franco Badian iliyopo kata Lumuma, Mkuu wa Wilaya amepongeza hatua ambayo shule hii imefikia kwa kukamilisha madarasa, kuweka tanki la maji, ujenzi wa vyoo vya kisasa na jinsi ramani ya shule ilivyopangwa vizuri ila ameuagiza uongozi wa shule hiyo kujenga jengo la utawala na viwanja vya michezo kwa kuwa watoto hucheza 50% na kusoma 50%.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri (Kushoto) akitoa maelekezo kwa uongozi wa shule Awali na Msingi ya Franco Badian iliyopo kata ya Lumuma (Picha Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA)
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa (aliyeinama) akiongea na wanafunzi wa shule Awali na Msingi ya Franco Badian iliyopo kata ya Lumuma (Picha Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA)
Mkuu wa Wilaya akifanya mkutano na kutoa maagizo kwa uongozi wa kata ya Lumuma katika eneo litakalotumika kuupokea Mwenge wa Uhuru (Picha Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA)
Kituo cha Afya Pwaga: Kituo cha Afya cha Pwaga kimefikia hatua ya lenta katika majengo yote kuanzia jengo ya wagonjwa wa nje (OPD), maabara, wodi ya akina mama, wodi ya upasuaji, mochwari na nyumba ya mganga mkuu wa kituo hicho. Aidha Mkuu wa Wilaya amepongeza hatua iliyofikia ila ameitaka kamati ya ujenzi na uongozi wa kata kwa ujumla kuwapa ushirikiano mafundi kwa kuwapatia mahitaji ya ujenzi ili waweze kukamilisha ujenzi kwa muda uliopangwa. Ambapo kwa mujibu wa mkataba kituo hicho kinatakiwa kumalizika tarehe 19 Juni 2018.
Mkuu wa Wilaya akiongea na kamati ya ujenzi pamoja na uongozi wa kata ya Pwanga kwenye jengo la wagonjwa wa nje (OPD) (Picha Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA)
Kituo cha wanyama kazi kibakwe: Hiki ni kituo ambacho wakulima na vikundi vya wakulima kutoka sehemu mbalimbali huwa wanakuja kujifunza masuala ya kilimo kama vile kupandiza, kilimo cha mboga mboga na matunda, jinsi ya kuzalisha mbegu, kuotesha kitalu cha mzao kama michungwa na korosho. Pia kituo hiko kina mashamba darasa ambayo huwawezesha wakulima kujifunza, kuna hosteli za kulaza wageni, kuna kompyuta za kutunza kumbukumbu na zimeunganishwa na mtandao wa internet.
Shughuli kuu katika kituo hiki ni kuwasaidia wakulima kuzalisha kwa tija kwa kuwapatie elimu na ushauri katika kilimo. Mazao yanayolimwa katika kituo hiki ni pamoja na nyanya chungu, hoho, cabagge, korosho, mahindi, bilinganya na bamia. Vile vile kuna miche inapatikana katika kituo hiki kama vile miche ya michungwa, korosho, na miembe iliyofanyiwa grafting na huanza kuzaa kwa muda wa mwaka mmoja tu.
Mkuu wa Wilaya (Kulia) akisikiliza taarifa fupi ya utekelezaji wa shughuli za kituo toka kwa msimamizi mkuu wa kituo hicho ndani ya ofisi ya kituo (Picha Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA)
Hosteli za kituo cha wanyamakazi - Kibakwe (Picha Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA)
Msimamizi wa kituo akielezea jinsi wanavyoweza kumwagilia kwa kutumia teknolojia ya Umwagiliaji kwa njia ya matone ( Drip irrigation) (Picha Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA)
Moja kati ya mashamba ya kituo yanayolikwa kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia teknolojia ya Umwagiliaji kwa njia ya matone ( Drip irrigation) (Picha Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA)
Mkuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na usala wamekipongeza sana kituo hicho kwa kuwa na mafanikio yanayoonekana na kuelezeka ila amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa wilaya ya Mpwapwa akiwezeshe kituo hiki kupata tanki la maji kubwa angalau lenye lita 5,000 ukilinganisha na la sasa ambalo ni dogo na maji yanaisha mapema kama alivyoeleza msimamizi wa kituo katika changamoto yao.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.