• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Mpwapwa District Council
Mpwapwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Mipango na Takwimu
      • Afya
      • Fedha na Biashara
        • Fedha
        • Biashara
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mali asili
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Vijana
      • Usafi na Mazingira
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Habari Mawasiliano na Tehama
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Nyuki
    • Mamlaka
      • Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mpwapwa
      • Mamlaka ya Maji Mpwapwa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Huduma za Uchumi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashuri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa mbali mbali
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo mbali mbali
    • Simulizi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video mbali mbali
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Habari

Mkuu wa Wilaya Atatua Mgogoro Sugu wa Ardhi

Posted on: December 31st, 2018

(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri leo ametatua mgogoro sugu wa ardhi uliodumu kwa muda wa mwaka mmoja mpaka sasa tangu ilipoletwa taarifa rasmi mwezi Disemba 2017. Katika kutatua mgogoro huu Mkuu wa Wilaya ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Paul Mamba Sweya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, timu ya wataalam toka Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa,  Wajumbe wa Kamati ya Halmashauri Kijiji cha Kibakwe, Viongozi wa kata,Tarafa na Walalamika (Wakulima).  Kutokana na hali ya mgogoro ilipofikia Mkuu wa Wilaya amelazimika kwenda katika shamba/eneo lenye mgogoro ili kujiridhisha mipaka ya shamba hilo lenye zaidi ya ekari 51.38.

Kiini cha Mgogoro huu ni baada ya wananchi wanne kutoka katika kijiji cha Kibakwe wakilalamika kuwa Serikali ya Kijiji cha Kibakwe na Kijiji cha Iyenge  inawazuia kulima katika mashamba yao ambayo wamekuwa wakilima kwa muda mrefu. Aidha mgogoro huu uliwasilishwa na walalamikaji katika Ofisi ya Mh. Mkuu wa Wilaya mwezi Desemba, 2017 na hatimaye ofisi hiyo iliiagiza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya kushughulikia mgogoro huo. Baada ya Ofisi ya Mkurugenzi kupokea mgogoro huu kutoka kwa walalamikaji na kupokea maelekezo ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, kikosi kazi cha kushughulikia migogoro ya ardhi ya Wilaya na watalaam wa Idara ya ardhi walielekezwa kushughulikia mgogoro huu akiwemo Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Ndug. Anderson Mwamengo.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri (wa pili kushoto) akiwa na wataalam wengine wakielekea katika eneo lenye mgogoro Katika Kata ya Kibakwe

Kutokana na maelezo ya pande husika na  mazingira ya eneo la mgogoro, chanzo cha mgogoro huu kinatokana na mvutano wa miliki na matumizi ya ardhi iliyopo ndani ya mipaka ya kijiji cha Iyenge. Kwa upande mmoja ardhi hiyo ipo katika mipaka ya kijiji cha Iyenge na kwa upande mwingine wananchi wanaotumia ardhi hiyo ni wakazi wa kijiji cha Kibakwe. Wananchi wanne wa kijiji cha Kibakwe ambao ni ndugu Mchiwa Bakari, Geophrey Chuguru, Selina Mbiduka na Damiani Mbiduka wanadai kuwa   Serikali za vijiji vya Kibakwe na Iyenge zinawazuia wasilime maeneo yao kwa madai kuwa eneo hilo lilikuwa ni shamba la kijiji, eneo la hifadhi Hifadhi ya Ardhi Dodoma (HADO) ambalo kwa sasa eneo hilo limetekwa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA).

Baada ya mgogoro huu kupokelewa, mnamo tarehe 20/01/2018 Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ilituma watalaam wa Idara ya Ardhi na wajumbe wa kikosi cha kushughulikia migogoro kufika katika kijiji cha Kibakwe na kuzikutanisha pande husika na mgogoro huo. Pia wajumbe wa Serikali ya kijiji cha Iyenge, viongozi na watalaam wa Kata ya Kibakwe na Afisa Tarafa wa Kibakwe walishirikishwa.

Kikao cha utatuzi kilifanyika katika ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Kibakwe, baada ya pande husika kukutanishwa na watalaam kutoka Wilayani walieleza kwa kifupi maudhui ya kikao hicho na hatimaye pande husika kupewa nafasi ya kutoa maelezo yao. Kwa hatua ya awali, walalamikaji ndio walianza kutoa maelezo ya malalamiko yao kama ifuatavyo:-

Mlalamikaji wa 1 ndugu Mchiwa Bakari

Mwananchi huyu alieleza kuwa, mwezi Desemba 2017 yeye na wenzake waliambatana  kwenda katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwenda kutoa taarifa juu ya mgogoro uliojitokeza baina yao na viongozi wa vijiji vya Kibakwe na Iyenge. Aliendelea kueleza kuwa mnamo mwezi Desemba, 2016 walipewa taarifa na Mtendaji wa kijjiji cha Kibakwe, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibakwe, Mtendaji wa Kata ya Kibakwe na Diwani wa Kata ya Kibakwe kuwa wasiendelee kulima mashamba yao kwa madai kuwa tumevamia eneo la ujenzi wa chuo cha VETA.

Pia ilielezwa kuwa; baadhi ya wananchi waliamua kulima bila kujali katazo walilopewa, mnamo tarehe 22/12/2016 wananchi wote waliokatazwa kulima eneo hilo waliitwa na kuelekezwa wafike kwenye  mashamba yenye mgogoro ili waoneshwe yalivyochukuliwa. Baada ya kufika mashambani inaelezwa kuwa  walioneshwa maeneo ya kutolima kwa vile ni sehemu ya maeneo ya HADO.

Baada ya kuona hakuna muafaka uliofikiwa katika eneo la mgogoro, mwananchi huyu anadai kuwa wao kama wamiliki wa mashamba yaliyochukuliwa na kijiji kwa matumizi ya ujenzi wa chuo cha VETA waliamua kuwasilisha malalamiko yao kwa Afisa Tarafa wa Kibakwe ili atatue mgogoro huo kama ulivyokuwa umejitokeza. Baada ya malalamiko kuwasilishwa kwa Afisa Tarafa, kiongozi huyo aliomba ufafanuzi wa na maelezo ya mgogoro huu kutoka kwa Mtendaji wa Kata ya Kibakwe, Mtendaji huyo alitoa ufafanuzi kuwa wananchi wenye mgogoro walikubali kutoa maeneo hayo ili yatumike kwa ujenzi wa chuo cha VETA. Hatimaye Afisa Tarafa alitoa maelekezo kuwa malalamiko ya wananchi hao yawasilishwe kwake kwa njia ya maandishi, kwa vile hawakujibiwa kwa wakati, hatimaye walalamikaji waliamua kwenda Wilayani kwa Mh. Mkuu wa Wilaya ili wasaidiwe kufikia ufumbuzi wa mgogoro huu.

Mlalamikaji wa 2 ndugu Damiani Mbiduka

Mwananchi huyu alieleza kuwa “eneo la mashamba yetu limechanganywa pamoja na eneo la VETA na HADO bila sisi wenyeji kushirikishwa, “aliendelea kutoa maelezo kuwa awali eneo la VETA lilikuwa ni shamba la kijiji, hata hivyo kuna wakati  shughuli za kilimo za kijiji zilizorota hivyo shamba liliachwa bila kulimwa. Baadae Serikali ilileta Mpango wa Hifadhi ya Mazingira uliojulikana kama HADO. Kijiji kiliamua kurudi katika eneo lake ambalo awali lilikuwa shamba la kijiji na kuanza kupanda miti. Alihitimisha kutoa maelezo kuwa yeye mwenyewe alianza kulima shamba lake mwaka 1985.

MAELEZO YA SERIKALI YA KIJIJI CHA KIBAKWE

Ndugu Mario Mnyanju – mjumbe wa Serikali ya kijiji cha Kibakwe

Mjumbe huyu  alitoa maelezo kama ifuatavyo;

“ Sisi kama kijiji cha Kibakwe tulipewa taarifa za kutenga eneo la VETA na uongozi wa Wilaya, tuliamua kushirikiana na kijiji cha Iyenge kutafuta eneo la ujenzi,  kwa vile mpango wa ujenzi wa chuo hicho ulikuwa ni wa Kata, wenzetu walishauri eneo la HADO ambalo lipo katika kijiji cha Iyenge tutenge eneo la ujenzi wa shule ya Kata. Baadae Iyenge walionesha mipaka ya HADO hivyo ilionekana eneo hilo linalimwa na wananchi wa kijiji cha Kibakwe. Awali wananchi wote waliokuwa wanalima eneo hilo waliondolewa lakini baadae walirudi na kuanza kulima. Baada ya kukubaliana kutenga eneo la VETA hapo, kijiji cha Iyenge walitutaka tuwajulishe wananchi wetu wasiendelee kulima katika ardhi hiyo. Pia ilionekana baadhi ya wananchi wa Iyenge wanalima katika eneo hilo.”

Maelezo ya mwananchi Gabriel Ngweitanile

Mwananchi huyu ambaye pia ni mstaafu aliyewahi kuwa mtumishi wa Umma, alitoa maelezo kuwa “mimi niliwahi kulima katika huko 5 years before we were stopped, baadae niliitwa na kijiji na kuelezwa kuwa eneo hilo ni la HADO, Mipaka ya HADO ilivyowekwa hatukushirikishwa tulikuwa tunaambiwa tu ondoka kwa ajili ya HADO.”

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri (wa kwanza kulia) akipata maelezo toka kwa Mlalamika/mwananchi Bakari Mwanamchiwa kuhusu eneo hilo lenye Mgogoro Katika Kata ya Kibakwe

MAELEZO YA AFISA TARAFA

Afisa Tarafa wa Tarafa wa kibakwe alitoa maelezo kama ifuatavyo;

“Wamiliki wote wa eneo liliotengwa kwa matumizi ya VETA walishirikishwa kuoneshwa mipaka, pia awali eneo hilo lilikuwa la HADO, shughuli za hifadhi ya mazingira zililegalega, wananchi wakarudi kwenye maeneo hayo, kwa sasa Serikali imechukuwa tena maeneo yake ili yatumike kwa ujenzi wa chuo cha ufundi cha VETA. Pia niliwahi kuwapa walalamikaji ufafanuzi huu lakini walionekana kutoridhika hivyo nikawaelekeza kama hawajaridhika wasonge ngazi za juu”.

KUTEMBELEA ENEO LA MGOGORO

Baada ya kikosi kazi na watalaam kupokea maelezo ya mgogoro kutoka pande zote, kwa pamoja ilikubaliwa kuwa, pande hizo pamoja na watalaam wafike eneo la mgogoro. Katika eneo la mgogoro wananchi hao wanne, kila mmoja alionesha mipaka ya eneo lake lilivyokaa, watalaam walichukuwa vipimo vya ardhini (coordinates) vya shamba la kila mwananchi na eneo lote la VETA. Kutokana na uhakiki wa ardhini ilibainika kuwa eneo lote la VETA lina ukubwa wa ekari 51.38 na mashamba ya walalamikaji yana ukubwa wa ekari 10.81. Eneo lisilokuwa na mgogoro lina ukubwa wa meta za eneo 40.57.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akiwa na wataalam wengine  kwenye eneo lenye mgogoro Katika Kata ya Kibakwe

 KILICHOBAINIKA

•Pande zenye mgogoro hazikubaliani  mpaka wa eneo la VETA na  Mashamba ya walalamikaji.

•Wakati wananchi wanne wamekatazwa na Serikali ya kijiji kulima katika eneo hilo, baadhi ya wananchi wengine wanaendelea kulima upande wa kasikazini wa eneo la

VETA.

•Eneo lote la mashamba na VETA lina uoto wa asili unaofanana, yaani mibuyu mikubwa.

•Eneo la mgogoro ni ardhi ya kijiji cha Iyenge, wanaolima ni wakazi wa kijiji cha Kibakwe.

•Eneo la mgogoro lina ukubwa wa ekari 10.81 eneo lote la VETA ni ekari 51.38

USHAURI WA KITALAAM

•Utengaji na upangaji wa ardhi unaofanywa na vijiji uheshimiwe.

Kwa vile Sheria ya Ardhi Na. 4 ya 1999, Kifungu cha (8) kifungu kidogo (1) – (8)huelekeza kuwa Halmashauri ya kijiji ndiyo chombo pekee cha kusimamia maslahi ya ardhi katika kijijiji na kuridhiwa na Mkutano mkuu wa Kijiji, zoezi la utengaji wa eneo hili kwa matumizi ya umma liheshimiwe na kulindwa kwa vile liliasisiwa n Serikali za vijiji vya Iyenge na Kibakwe na hatimaye kuridhiwa na vijiji, Kata, Tarafa na Wilaya.

•Wananchi wote wanaolima eneo la VETA wajulishwe kulima  msimu huu, msimu unaofuata wasilime tena, eneo libaki wazi kwa matumizi ya umma.

•Eneo lote la VETA lipimwe na kuwekwa alama za kudumu (beacons)  za  upimaji ili kuzuia uvamizi kwa siku za baadae.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri (wa pili kulia) akipawe maelezo toka kwa Afisa Ardhi na Maliasili Ndug. Anderson Mwamengo juu ya Mipaka ya eneo lenye mgogoro  Katika Kata ya Kibakwe

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Shekimweri baada ya kusomewa taarifa ya mgogoro huu na Afisa Ardhi na Maliasili Wilaya Ndug. Anderson Mwamengo, kusikiliza maelezo ya walalamikaji, maelezo ya viongozi wa kijiji na kata, na kukagua eneo hilo amebaini yafuatayo:-

Eneo lenye mgogoro halina mipaka inayotambulika yenye alama za kudumu (beacons).

Eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Chu cha VETA lina ukubwa wa ekari 51.38 wakati sheria haiirusu kijiji kumilisha taasisi au mtu eneo  lenye ukubwa zaidi ya ekari 50.

Eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA ni kubwa sana, kitaala Chuo cha VETA kwa Mijini hutosha kujengwa kwa ekari 16 tu.

Kutokana na kubaini haya, Mkuu wa Wilaya ameamua wananchi/walalamika (wakulima) wanne wapewe maeneo yao ambayo yenye jumla ya ukubwa wa ekari 10.81.

"Naagiza wakulima hawa wanne kuanzia sasa ndio wamiliki halila wa eneo hilo walikuwa wamezuiwa kulima na Afisa  wa Ardhi Wilaya anza taratibu za kuwapatika hata hati za kimila

ili wasisumbuliwe tena", amesisiti Mhe. Shekimweri.

Pia Mkuu wa Wilaya amemuagiza Afisa Ardhi kupima eneo lote lililotengwa kwa ajili ya Chuo cha VETA lenye ekari 40.57 zilizobaki baada ya kutoa maeneo ya wakulima na kuweka alama za kudumu.

Kwa maelezo zaidi pakua nyaraka hii:-

Taarifa ya Mgogoro wa Ardhi Kijiji cha Kibakwe na Iyenge.pdf

Matangazo

  • Tangazo la kuitwa kwenye usahili MpwapwaDC June 27, 2022
  • Tangazo la nafasi za kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. 2022 April 20, 2022
  • Tangazo la Nafasi za Kazi Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa May 2022 May 31, 2022
  • Tangazo la kuahirishwa kwa Usahili Halmashauri ya Mpwapwa June 22, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • NORISH NA WAKULIMA WILAYA YA MPWAPWA

    May 06, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR WATEMBELEA MIRADI YA MFUKO WA JIMBO MPWAPWA

    May 09, 2025
  • FUM YAFANYA ZIARA MIRADI YA KIMAENDELEO

    April 29, 2025
  • MAADHIMISHO YA MEI MOSI YAFANYIKA SINGIDA

    May 01, 2025
  • Tazama zote

Video

Video ya Mpango wa Uuzaji wa Viwanja Eneo la Mazae Block "E" katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa -2020
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
  • Muundo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani
  • Ratiba ya Vikao vya Madiwani

Viunganishi Linganishi

  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Wizara ya Fedha na Mipango
  • Utumishi portal
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu Teknolojia na Sayansi
  • Sekretarieti ya Ajira

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mpwapwa - Dodoma, Tanzania

    Anwani: S.L.P 12

    Simu: 255 26 2320122/2320

    Simu ya Kiganjani: 0684705551

    Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovutii

Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.