Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri leo katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kilichofanyika katika Ukmbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ameliambia Baraza hilo kuwa anaimani kubwa kwa sasa na utendaji wa Mkuregenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Maneno hayo yamejili baada ya wenyevit wa kamati mbalimabli kuwasilisha taarifa zao ikiwepo kamati ya Fedha Uongozi na Mipango (FUM) kuwasilisha taarifa ya hali ya Ukusanyaji wa mapato na kuongezeka kwa mapato.
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa wakiwa kakiimba Wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Madiwani
Mhe. Kimweri ameeleza kuwa "Nia yangu ni kuiona Halmasahuri ya Wilaya ya Mpwapwa inasongambele katika ukusanyaji wa mapato na kuthibiti mianya ya upotevu wa mapato, hakika katika mapato nitasimamia kwa thati. Kwanza nimpe pongezi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmasshauri ya Wilaya ya Mpwapwa na Menejimenti yake pamoja na waheshimiwa madiwani kwa kushirikiana kuweka mikakati mizuri ya ukusanyaji wa mapato, mapaka sasa ni robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019 Mpwapwa imefikia alisimia 33.4 na imevuka lengo la asilimia 25 kwa kila robo mwaka." Ameongeza kuwa hapa sasa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa inaenda vizuri katika ukusanyaji wa mapato na tutafikia malengo yetu.
Pia Mkuu wa Wilaya ameonya kuwa atakuwa makali na kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtumishi au mtu yeyote atakayehujumu jitihada za ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
Vile vile ameeleza jitihada alizozifanya katika kuunga mkono katika suala ukusanyaji na uthibiti wa mapato ni pamoja na Kwenda Dar es Salaam kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Dayone Softcom Technologies kununua POS 30 aina ya TELPO TPS 390 kwa mali kauli (mkopo) na kuruhusu askari polisi kushirikiana na wataalam wa Halmashauri katika kuthibiti utoroshaji wa mapato wakati wa usiku.
Mheshimiwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya akimuapisha Mhe. Diwani wa Kata ya Wangi baada ya diwani wa kwanza kufariki.
Mkuu wa Wilaya ametoa taarifa Kliniki Tembezi iliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa kuanzia tarehe 21 Octoba hadi 28 Octoba 2018 ambapo madaktari bingwa pamoja na wasaidizi wao toka Dodoma Hospitali ya Mkoa, Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma na Muhimbili walifika na jumla yao ilikuwa zaidi ya 70 na walifanikiwa kutoa tiba kwa wagonjwa zaidi ya 2,000 wenye magonjwa mbalimbali. Mhe. Kimwei ameomba Idara ya Afya iendelee kuratibu zoezi hili ili liweze kuendelea kwa kipindi kingine kwa sababu inaonyesha wananchi wanahitaji kwa wingi huduma hii.
Aidha amewatangazia fursa madaktari bingwa ya kilimo cha korosho katika Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa na amewahaidi kila daktari atapewa ekari moja bure, Madaktari bingwa hao wamekubali kuanza kilimo cha korosho Mpwapwa na kwa kuanzia kila daktari amehitaji ekari 10 kwa kununua japo kila mmoja atapewa ekari moja bure. Mpaka sasa madaktari bingwa wanaohitaji kulima kilimo cha zao la korosho Mpwapwa wamefikia 100 na wengine wanaendelea kutoa ahadi ya kuhita mashamba.
Waheshimiwa madiwani wakiwa katika kikao cha Baraza la Madiwani
Pia, Mkuu wa Wilaya ametoa wito kila kata na taasisi za serikali kuanzisha mashamba ya zao la korosho na kuweka sheria ndogo kwa wale watakaoharibu au kulishia mifugo katka mashamba ya korosho na kusababisha uharibifu wa mikorosho hatua zichukuliwe dhidi yao.
Kutokana na ushaushi huu wa Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmasahuri ya Mpwapwa Mhe. Donath S. Nghwenzi amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuijali na kuwa na nia njema na Wilaya ya Mpwapwa na amehaidi kusimamia kikamilifu masuala yote muhimu na kuzingatia ushauri uliotolewa na Mkuu wa wilaya katika zao la korosho na ukusanyaji wa mapato.
Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.