Mkuu wa Walaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri, amemuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Mpwapwa kutembelea miradi ya Vituo vya Afya vya Mima, Kibakwe na Pwaga vinvyoendelea kujengwa, ambapo Kaimu Mkurugenzi huyo amewakilishwa na Afisa Mipango wa Wilaya Ndg. Dismas Pesambili. Aidha Mkuu wa Wilaya ametaka kupata taarifa za kina kuhusu maendeleo ya ujenzi na changamoto zinazowakabiri kamati za ujenzi na watendaji kwa ujumla iliziweze kutatuliwa mara moja na kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Agizo hili limejili kwa kuwa Mkuu wa Wilaya ameshindwa kuambatana na timu ya Kaimu Mkurugenzi kwenda kutembelea miradi hiyo kutokana na majumu mengine muhimu ya kiofisi kumbana na kuamua kutoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi.
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi huyo ametii agizo hilo kwa kutuma timu ya wataalam kwenda kutembelea miradi hiyo, timu hiyo imemhusisha Afisa Mipango wa Wilaya, Mhandisi wa Ujenzi Wilaya Ndg. Yesse na Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Ndg. Lymo ambao kwa pamoja wametembelea na kukagua ujenzi wa Vituo vya Afya hivyo. Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi ameipongeza kamati ya ujenzi kwa hatua iliyofikiwa na kumtaka mkandalasi kwendana na muda, hivyo aongeze bidii ili amalize kwa wakati.
Akielezea mkandalasi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Mima, kuwa nyumba ya mganga, imekamilika kilichobaki ambacho kinamaliziwa sasa ni vitasa vya milango na baadae kumalizia mashimo ya vyoo. Pia ameongeza kuwa katika jengo la maabara bado madirisha, ngazi za kuingilia na mashimo ya vyoo ambavyo ndani ya wiki hii vyote vitakamilika.
Vilevile Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi na timu yake walipata fursa ya kutembelea jengo la upasuaji, wodi ya akina mama na wodi ya watoto, ambapo zote zinaendelea kujengwa.
Nyumba ya Mganga katika kituo cha Afya Mima
Jengo la Maabara na hatua ilipofikia sasa, Kituo cha Afya Mima
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi (watatu toka kushoto) akitoa maelekezo kwa kamati ya ujenzi, kwenye jengo la wodi ya watoto ambalo lipo katika hatua ya jamvi - Mima
Jengo la Upasuaji katika kituo cha Afya Mima
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi (wa kwanza kulia) akiwa na timu yake kukagua Wodi ya akina mama katika kituo cha Afya Mima.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.