Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Lumuma Kijiji cha Kitati Wilayani Mpwapwa. Mkutano huo umefanyika kwa lengo kurejesha mrejesho wa Tume huru ya Uchunguzi iliyoundwa na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa kuchunguza tuhuma za ubadhilifu wa fedha za mradi wa Ujenzi wa Mfereji wa Umwagilia unaofadhiliwa na LIC katika Bonde la Lumuma kijiji cha Kitati. Katika tuhuma hizo wananchi wa Kitati waliwatuhumu viongozi wa kijiji na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ujenzi wa mfereji kuwa wamekula fedha za mradi ndio maana mradi unasuasua kukamilika.
Wananchi wa Kijiji cha Kitati wakisikiliza kwa umakini Taarifa ya Tume ya Uchunguzi iliyoundwa na Mhe. Jabir Shekimweri Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa
Akisoma taarifa yaTume ya Uchunguzi huo Bi. Julieth Mtuy ambaye Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Mpwapwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, wananchi wa kijiji cha Kitati, viongozi toka Wilayani na Wadau mbalimbali wa kilimo walioambatana na msafara huu.
Katika taarifa ya Tume ya Uchunguzi imebaini kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Mfereji Bw. Hamza Mkude ameiba mifuko 6 ya saruji na Bw. Shedrack Msangi ambaye ni Mtunza vifaa vya mradi katika Taarifa ya Tume ya Uchunguzi imemtaja mtunza vifaa huyo ameiba mifuko 32 ya sarufi. Vile vile tume imebaini kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kamati ya ujenzi walikamatwa na kupigwa faini ya kiasi cha Shilingi Laki Mbili (Tsh. 200,000/) kila mmoja kimakosa na uonevu kwa kuwa viongozi hao walikuwa wasimamizi wazuri wa mradi na walikuwa wanafuatilia hatua moja hadi nyingine ya mradi huo.
Tume ya Uchunguzi imependekeza kuwa waliobainika kuiba mifuko ya saruji walipe mara moja, waliopigwa faini warudishiwe fedha zao na warudishwe katika nyazifa zao ili waendelee kusimamia maradi wa ujenzi wa mfereji na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kitati Bw. Amon Mdajile ahamishwe kituo cha kazi kwa kuwa amekaa muda mrefu na ameshindwa kusimamia mradi huo.
Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Mpwapwa Bi. Julieth Mtuy akisoma taarifa ya Tume ya Uchunguzi mbele ya Mkuu wa Wilaya, wadau wa Kilimo na wanachi wa kijiji cha kitati
Baada ya taarifa kusomwa, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri ametoa agizo la kukamatwa Bw. Hamza Mkude amabaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi na kulipa mifuko yote 6 ya saruji aliyoiba, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kitati ahamishwe na kwa kuwa hakutoa ushirikiano katika zoezi la uchunguzi na Bw. Shedrack Msangi akamatwe na kulipa mifuko 32 ya saruji aliyoiba.
Mhe. Shekimweri amesisitiza kuwa "Sina utani katika masuala ya maendeleo na mambo yanayowagusa wananchi moja kwa moja, kwa hali hii siwezi kuvumilia; nilifanya mkutano hapa Kijiji cha Kitati na niliwahaidi kuwa nitaunda Tume ya Uchunguzi na majibu yake ndio haya, hakuna aliyeonewa hapa kila mhusika alihojiwa na kutoa maelezo yake. Sasa hawa watu watatu Bw. Hamza Mkude, mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Bw. Shedrack Msangi mtunza vifaa (mtunza stoo) na Bw Amon Mdajile Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kitati leo naondoka nao, OCD (Kamanda Mkuu wa Polisi Wilaya) kamata hawa".
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri akitoa agizo la kukamatwa kwa wahusika walioiba mifuko ya saruji iliyokuwa ikitumika katika ujenzi wa mfereji kijiji cha Kitati
Diwani wa Kata ya Lumuma Mhe. Joctan Cheliga katika hotuba yake ya shukurani amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuunda Tume na kubaini haya, na amewasihi wananchi wa Kitati kuwa waaminifu katika kusimamia miradi ya maendeleo ya wananchi kwa kuwa miradi hii ina manufaa kwa wanakijiji cha Kitati.
Diwani wa Kata ya Lumuma Mhe. Joctan Cheliga akitoa neno la shukurani kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.