Na: Shaibu J. Masasi; Afisa TEHAMA - Mpwapwa Dc
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri leo ameamua kutembelea baadhi Taasisi za Umma ili kujionea na kupata taarifa jinsi wanavyotekeleza maagizo ya Serikali jinsi ya kujikinda na maambukizi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID-19). Mhe. Shekimweri akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ametembelea na kukagua vifaa vilivyowekwa ili kujikinda na maambukizi dhini ya corona katika taasisi za Chuo cha Mifungo (LITA), Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TARILI), Chuo cha Afya, Chuo cha Ualimu Mpwapwa, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka ya Maji.
Aidha katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya amepata fursa ya kuongea na watumishi na kutoa maelekezo ya Serikali ikiwemo kila Mtumishi nyumbani kwake aweke ndoo ya maji safi yanayotiririka na sabuni, kutopokea wageni wanaotoka katika mikoa au Nchi zenye ugonjwa wa Corona-19 bila kuwa na tahadhali, kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kama itatokea mikusanyiko ya lazima kila mmoja anapaswa kukaa angalau mita moja toka mtu mmoja hadi mwingine, kunawa mikono mara kwa mara kwa maji safi yanayotiririka na sabuni, kutowanyanyapaa wagonjwa wa corona endapo watabainika, kutoa taarifa kama kuna mtu ana dalili za corona, kutokuwa na hofu ila kuchua tahadhari, kutoa elimu ya ugonjwa wa corona kwa familia na majirani wanaowazunguka.
Vilevile amewapongeza Wakuu wa Taasisi na watumishi wote katika taasisi alizotembelea kwa kuona ndoo za maji safi yanayotiririka na sabuni, na kuelekeza kwa vitendo jinsi ya kunawa mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni. Pia amewataka wakuu wa taasisi kuweka koki zinazoweza kufunguliwa kwa kiwiko cha mkono na sio kwa vidole kwa sababu wakati wa kufungua unweza kuacha uchafu na wakati wa kufunga ukachukua uchafu.
Akisisitiza maagizo ya Serikali Mhe. Shekimweri amesema "hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kutoa taarifa ya kuthibitisha kuwepo kwa mgonjwa wa corona au takwimu ya wagonjwa wa corona dhini ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tu".
Mkuu wa Wilaya (aliyeinama) Akitoa Maelekezo kwa Vitendo jinsi ya Kunawa Mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni katika Chuo cha Mifungo (LITA),
Mkuu wa Wilaya (kushoto) Akiangalia muda wa kuisha (expire date) ya sabuni ya maji katika Chuo cha Ualimu Mpwapwa,
Mkuu wa Wilaya (aliyeinama) Akitoa Maelekezo kwa Vitendo jinsi ya Kunawa Mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Mkuu wa Wilaya (aliyeinama) Akitoa Maelekezo kwa Vitendo jinsi ya Kunawa Mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni katika taasisi ya Mamlaka ya Maji
***Mwisho***
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.