Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri leo amekagua hali ya uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji katika kijiji cha Lwihomelo kata ya Wangi wilayani Mpwapwa. Katika ukaguzi huo Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa amebaini uharibifu mkubwa wa chanzo kikuu cha maji kinachotiririsha kwenda katika kidakio cha maji kilichopo kata ya Kibakwe.
Uharibifu huo umesababishwa na kilimo kisichozingatia kanuni bora za kilimo, sheria ya usimamizi wa rasilima za maji na sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 kifungu cha 57 (1).
Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ameagiza wananchi wote waondolewa katika eneo hilo la chanzo cha maji na eneo hilo lipandwe miti, nyasi rafiki kwa maji na kuliwekea mipaka ndani ya siku saba.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri (kushoto) akipanda nyasi rafiki kwa maji katika mfereji wa chanzo kikuu cha maji kinachotiririsha maji kwenda kata ya Kibakwe (Picha: Theodory Mulokozi - Afisa Mazingira, Mpwapwa)
Wataalam waliombana na Mhandisi wa Mjai Bi. Christina Msengi (kushoto waliokaa chini) wakiwa katika kidakio cha maji cha kata ya Kibakwe wakijadili jambo.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri (watatu kulia) akipata maelezo toka kwa Kaimu Afisa Mtendaji wa kata ya Wangi juu ya hali ya uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji (Picha: Theodory Mulokozi - Afisa Mazingira, Mpwapwa)
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.