(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri leo amewahamasisha wananchi wa Mpwapwa kufanya mazoezi ya viungo na riadha kama ilivyokawaida kila Jumamosi ya wiki ya pili ya kila mwezi kuwa na mazoezi ambayo yamefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chazunga Wilayani Mpwapwa.
Aidha katika mazoezi ya leo yamehudhuriwa na Katibu Tawala wa Wilaya Ndug. Sarah Komba, Afisa Usalama wa Taifa Ndug. Said, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpwapwa Ndug. Paul Mamba Sweya, wakuu wa idara, taasisi pamoja na wananchi kwa ujumla, wamefanya mazoezi ya ziungo kwa pamoja.
Mazoezi hayo yameongozwa na Mwalimu wa Michezo ambaye pia ni Afisa Utamaduni na Michezo Wilaya Ndug. Waziri Lwimbo kwa kutoa mazoezi mbalimbali ya viungo kwa watu wote waliohudhuria katika Viwanja vya Chazungwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri (wa tatu kulia), Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Sarah Komba (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Paul Sweya (wa kwanza Kulia) wakiwa katika mazoezi ya viungo kwenye Viwanja vya Chazungwa kata ya Mpwapwa Mjini.
Baada ya kumaliza mazoezi Mkuu wa Wilaya amepata fursa ya kuzungumza na wananchi waliohudhuria katika mazoezi hayo kuwa "Kwanza nimefurahishwa sana na mwitikio mkubwa wa watu kujitokeza kwa wingi katika kuthamini mazoezi, hii inaonyesha kuwa elimu na hamasa iliyotolewa juu ya mazoezi ni tiba kiafya imeanza kueleweka vizuri. Kwa ujumla mazoezi ni tiba kiafya na mara nyingi husaidia kuondoa msongo wa mawazo, matatizo ya shinikizo la damu (blood pressure) na kuuweka mwili kuwa imara wakati wote" ameeleza Mkuu wa Wilaya Mhe. Shekimweri.
Pia ameongeza kuwa anawashukuru wakuu wa taasisi, idara, vitengo na wananchi kwa ujumla kuhudhuria katika mazoezi haya na kusema kuwa "Afya ni Mtaji wetu katika kufanyakazi kwa kuwa imara bila maradhi".
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri akizungumza na wananchi waliohudhuria katika mazoezi ya viungo kwenye Viwanja vya Chazungwa kata ya Mpwapwa Mjini.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa amezindua Klabu ya Riadha ya Kikundi cha Mtaa wa Kikombo Road katika Kata ya Mpwapwa Mjini Wilayani Mpwapwa. Uzinduzi huo umefanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chazungwa mara tu baada ya mazoezi kumalizika. Kikundi hiki kinachojulikana kwa Jina la Kikombo Road Jogging Club kimeanzaishwa na wanachama wa kikundi hicho wapatao 20 na kinafadhiriwa na Ndug. Said, Afisa Usalama wa Taifa Wilaya ya Mpwapwa pamoja na Ndug. Sarah Komba, Katibu Tawala Wilaya ya Mpwapwa. Kikundi hiki kilianzishwa tangu mwaka 2018 baada ya Serikali kutoa tamko la kuwa na Mazoezi kwa wananchi wote Nchini kwa siku ya jumamosi ya wiki ya pili ya kila mwezi ili kuunga mkono jitihada za viongozi wa Serikali za kuanzisha siku maalum kwa ajili ya mazoezi. Pia kikundi kunajihusisha na michezo ya mpira wa miguu, kikapu, riadha na mazoezi ya viungo. Kikundi hiki kina malengo ya kuanzisha michango ya ihari, kujifunza michezo mbalimbali, nje ya wilaya akaunti, kufanya mashindando na vikundi vingine vitakavyoundwa ndanina nje ya wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe. Jabir Shekimweri, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Sarah Komba na Afisa Usalama Wa Taifa Wilaya ya Mpwapwa Ndug. Said pamoja na Wanachama wa Kikombo Roaad Jogging Club wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya uzinduzi wa club hiyo kwenye Viwanja vya Chazungwa kata ya Mpwapwa Mjini.
Mkuu wa Wilaya ametoa rai kwa wananchi wa Mpwapwa kuunda Jogging Club kila mtaa na hapa anasema "Natamani kila mtaa kuwa na Jogging Club mfano Mtaa wa Mwanakianga, Igovu, National, Majengo, Mji Mpya nk. Mimi nitakuwa bega kwa bega nanyi kwa namna yoyote ya kuunga mkono suala hili".
Mkuu wa Wilaya ametoa Wito kwa viongozi wote wa mitaa kuanzisha Jogging Club katika mitaa yao kwa kuwahusisha wananchi na watumishi wote wanawake na wanaume.
Walimu wa michezo Ndug. Waziri Lwimbo (kusho) na Ndug. Mchasi (kulia) wakitoa mazoezi ya viungo katika Uwanja wa Chazungwa Mpwapwa Mjini
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.