Mkutano wa Wadau wa Elimu wilayani Mpwapwa hufanyika kila mwaka na ulianza rasmi mwaka 2017, ila kwa mwaka huu 2018 pamoja na mambo mengine mkutano huu ulihusisha wadau mbalimbali kama vile viongozi wa serikali, wanasiasa, taasisi, dini, wafanyabiashara, walimu, wafanyakazi wa kada zote, wanafunzi na vijana toka Chuo Kikuu cha Dodoma ambao ni wazawa wa Mpwapwa.
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Ndg. Jabir Shekimweri akitambulisha meza kuu katika Mkutano wa Wadau wa Elimu kwenye Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mpwapwa.
Madhumuni ya Mkutano huu ni kutathmini matokeo ya mitihani (darasa la nne, la saba, kidato cha pili na kidato cha nne), kuibua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na kuweka mikakati ya kuzitatua changamoto hizo kwa kupata mawazo mbalimbali toka kwa wadau wa elimu. Katika tathmini ya matokeo ya mitihani ya mwaka 2017: shule, kata, walimu na wanafunzi waliofanya vizuri walipata zawadi mbalimbali kama vile pesa taslim, vitambaa vya suti, vyeti, vyombo vya nyumbani na luninga. Pia shule na kata zilizofanya vibaya walituzwa bendera nyeusi na vinyago kama ishara ya kufanya vibaya na wanahimizwa kujitahidi ili kupata matokeo mazuri.
Wadau wa Elimu wakiwa katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mpwapwa tayari kwa Majadiliano
Katika mkuto wa mwaka huu Mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge ambaye katika hotuba yake alipongeza kuanzishwa kwa mkutano wa wadau wa Elimu na ameziagiza Halmashauri zote za mkoa wa Dodoma kufanya mkutano kama huu kabla ya mwishoni mwa mwezi Januari mwaka 2018 kama huu ili kubaini changamoto za elimu na kuzitafutia uvumbuzi. Aidha amesema kuwa elimu ni ya msingi sana hivyo wazazi na wadau mbalimbali wawekeze kwenye elimu kwa kuwawezesha wanafunzi katika chakula na mahitaji muhimu kwa kuwa serikali inatoa Elimu bure.
Pia ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa kwa kufanya vizuri katika jitihada za kuinua taaluma, akitolea mfano katika matokeo ya mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi (darasa la saba) mwaka 2017 wilaya ya Mpwapwa ilishika nafasi ya 2, kwa kufaulisha 63.68% kimkoa wakati mwaka 2016 ilipata 58.4% ilishika nafasi ya 7 kimkoa, aidha amelezela kwa upande wa Elimu sekondari katika matokeo ya kidato cha pili mwaka 2017 ufaulu ulikuwa 92%.
Vile vile amesema kuwa anazifahamu changamoto za madawati, madarasa, upungufu wa walimu, utoro na mimba, hivyo wadau wa elimu wa wajadili namna ya kutatua changamoto hizo kwa kubuni mikakati mipya ya kutatua. Pia amependekeza walimu wanatakiwa kuhamishwa kwenda katika maeneo ambayo hayana walimu wa kutosha kwakuwa kuna baadhi ya shule na halmashauri zina walimu wa ziada wengi.
Sambamba na hilo ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Mpwapwa kutembelea maeneo ya kutolea huduma kwa maana shule ili kubaini changamoto zinazozikabili shule na kuzitatua mara moja ili kuwatia moyo wa kufanyakazi kwa bidii.
Wadau wa Elimu wakiwa katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mpwapwa wakisikiliza kwa umakini hotuba ya Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Dodoma.
Bofya hapa chini kupata hotuba mbalimbali.
Tathmini ya matokeo ya idara ya elimu msingi katika mkutano wa wadau wa elimu Januari 2018.ppt
Tathmini ya matokeo ya idara ya elimu sekondari katika mkutano wa wadau wa elimu Januari 2018.pptx
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.