"Fuga Kitaalamu, Lima Kitaalamu, Tumia Maarifa"
Ni kauli mbiu iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Mahenge, alipotembelea Wilaya ya Mpwapwa hivi karibuni. Pamoja na mambo mengine ameongea na watumishi pamoja na kutembelea taasisi mbalimbali. Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wadau wa elimu kushirikiana katika kuboresha elimu ili wananchi waelimike na hatimaye wanufaike na ujio wa serikali mkoani Dodoma. Mambo mengine ya Msisitizo ni pamoja na wakulima kujikita katika kilimo bora chenye kuzingatia kanuni na maarifa ili malighafi kwaajili ya viwanda ziweze kuzalishwa kwa wingi. Amezitaka Halmashauri zilizopo katika Mkoa wa Dodoma kubainisha Fursa za Uwekezaji, kutatua migogoro ya ardhi na kushughulikia kero za wananchi kwa wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Mahenge akiwahutubia watumishi wa taasisi mbali mbali Wilayani Mpwapwa katika Ukumbi wa Mkuu wa Wilaya tarehe 10.11.2017
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.