(Na: Shaibu J. Masasi, Afisa TEHAMA - Mpwapwa)
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Binilith S. Mahenge leo ameusifia uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa kunzia Mkuu wa Wila ya Mpwapwa, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa pamoja na Mkuu wa Idara katika kusimami matumizi ya fedha za miradi na kuwa na miradi iliyokamilika. Akitolea mfano wa katika usimamizi wa ujenzi wa Vituo vya Afya vya Kibakwe, Pwaga na Mima. Vilevile katika ujenzi unaendelea wa vituo vya Afya vya Mtera na Chipogo wenye gharama ya zaidi ya Tsh 600,000,000/= kwa pamoja ambapo vituo vya afya vinaendelea vizuri.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo katika kikoa cha Baraza la Madiwani la Mpwapwa cha kujadili hoja za Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa.
Wajumbe wakifuatilia majibu ya Hoja za Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/2020.
Pia amepongeza kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kupata hati safi katika Ukaguzi wa Mwaka wa Fedha 2018/2019. "Kupata hati safi inaonesha kuwa hakuna dosari kubwa
zilizofanyika katika usimizi wa fedha na utekelezaji wa majuku katika kuwahudumia wananchi". Akiwasilisha kwa ufupi Mkurugenzi wa Halmasahuri ya Wilaya ya Mpwapwa kuwa "Hoja saba zilikuwa hazina majibu na viambatanisho, hadi leo haoja hizo zimepetiwa majibu na zimeshawasilishwa kwa mkazi kwa ajili ya uhakiki".
Hata hivyo pamoja na hoja hizo saba zilikuwa hazijajibiwa lakini Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imepata Hati safi. Hoja hizo zilizokuwa hazina majibu ya kurithisha ni pamoja na: Usimamizi wa mapato, kutokulipwa kwa madeni ya Halmashauri, kuongezeka kwa mali za kudumu za Halmashauri, Kuthibiti Kesi za Halmashauri, Kuwepo kwa magari mabovu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mikakati ya Ukarabati wa Majengo ya shule za msingi na sekondari, Madawa yaliyoisha muda wake yanayotakiwa kuharibiwa,
Hata hivyo hoja hizo saba zimepatiwa majibu na kuwasilishwa kwa CAG kwa ajili ya uhakiki.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amepongeza sana katika Usimamizi wa Mapato na kufikia 121 kwa mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Tango niingie dodoma wilaya ambayo zimetengewa fedha na kazi zimeenda vizuri ni wilaya ya mpwapwa. Aidha sehemu zingine ukiona miradi haiendi ni kwasasabu ya 10% au maslai binafsi lakini kwa mpwapwa sijaona kitu kama hicho, nawapongeza sana madiwani wa mpwapwa na uongozi mzima wa wilaya kwa usimamizi mzuri.
Pia Mkuu wa Mkoa, Hizi hoja zinazalishwa na wakuu wa idara husika, hivyo tunahiji kuwa na mikakati ya kufuta hoja hizo na kuzuia kuzalisha hoja, zibaki zile za kisera kama uhaba wa watumishi.
Naye Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Kanda ya Dodoma Ndugu. Chami ameeleza namna ambavyo alivyopata ushirikiano kwa wakuu wa idara na vitengo wakati wa ukaguzi na kuwa kuwasilisha
nyaraka kwa wakati na kutoa maelezo yaliyojitosheleza. Pia ameomba kuwa wakatika wa ukaguzi nyaraka zote zinazohitajika zifike kwa wakati ili kuepuka kuwa na hoja nyingi zinazoweza kufutika.
Mwisho mkuu wa Mkoa ameahidi kuzifuanyia kazi hoja za kisera na kisekta ili ziweze kufutwa.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.