Mkutano wa kujadili Mradi wa Uboreshajia Salama wa milki za Ardhi (LTIP)umefanyika katika ukumbi wa CCM wilayani Mpwapwa ulibeba kauli mbiu isemayao “Usawa wa kijinsia katila umiliki wa ardhi kwa ustawi wa jamii”
Lengo kuu la mkutano huo ni kujadili mradi na uboreshaji usalama wa milki za ardhi.
Sambamba na hayo Mkurugenzi Mtrndaji wa Halmshauri Bi:Mwanahamisi H.Ally amewaomba wataalam kuandaa ofisi ili waweze kufanya kazi kwa umahiri na kujituma ili kazi iweze kuwa nyepesi.
Halikadhalika Mgeni rasmi Diwani wa kata ya Mpwapwa Mjini Mh.George O.Fuime akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa amesisitiza kutokuwa na ubabaishaji katika upimaji wa ardhi kwa kupitia mradi huu,pia amewaomba kuwa makini ili wananchi waweze kupata haki zao huku akisisitiza kwamba Wilaya yay a Mpwapwa ina sehemu nyingi sana zenye Madini lakini hazijapimwa,hivyo kupitia mradi huu yapimwe ili wananchii wapate stahiki zao.
Katika Halmshauri ya Wilaya ya Mpwapwa takribani hatimiliki 30,059zitatolewa katika kata zipatazo saba ambapo kila kiongozi katika kata yake anapaswa kushiriki zoezi kikamilifu ili kuhakikisha inafanyika kwa ufanisi na kwa wananchi jukumu lao ni kuhakikisha wanatoa taarifa kwa usahihi kwa wataalamu.
Mkutano huo umefanyika Juni 18,2024 huku ukifikia makubaliano yaliyotokana na majadiliano mbalimbali ya wadau waliohudhuria katika amakutano.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.