Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi H Ally amesisitiza suala la Usafi,kutunza Mazingira ili kuweza kuzipa taka thamani kwa Wanaberege na jamii kwa ujumla wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani.
Wito huo ameutoa leo Septemba 20,2025 wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Berege yalipofanyika maadhimisho hayo Kiwilaya.
"Suala la usafi tulipe kipaumbele kwenye jamii zetu kuanzia kwenye Taasisi,Mashuleni na Manyumbani mwetu"Amesema Bi Mwanahamisi
Halikadhalika, amewakumbusha suala la kufanya usafi wa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi,siku ambayo iliasisiwa na Hayati Jonh Pombe Magufuli Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuipa siku hiyo kipaumbele na kusisitiza Usafi wa kila mwisho wa mwezi ili tuweka Mazingira mazuri.
"Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku ya Usafi"
"Kila wakati tunatakiwa kufanya usafi ile siku imewekwa tu kwa ajili ya kufanya usafi wote kwa pamoja na kuhakikisha tunafanya usafi wa nguvu" amesema Mkurugenzi.
Maadhimisho haya ya Siku ya Usafi Duniani yameadhimishwa na Kauli Mbiu isemayo
"Tokomeza taka za Plastiki,Jengaa Jamii yenye Afya Bora"
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: 0684705551
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.