Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi H Ally akiongozana na wakuu wa idara na vitengo leo Januari 09,2025 amefanya ziara ya kikazi ya kukagua Miradi ya kimaendeleo inayoendelea kujengwa wilayani Mpwapwa.
Lengo la ziara yake hiyo ni kuweza kutambua maendeleo ya miradi hiyo na hatua iliyofikia pamoja na kutolea ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazojitokeza wakati ujenzi ukiendelea.
Wakati wa ziara yake hiyo amekagua mradi wa Shule mpya ya Sekondari ya Amali ya Mmbuyuni Kata ya Mpwapwa Mjini ,mradi wa Shule ya Sekondari Kimaghai 'A',ujenzi wa Shule ya Sekondari Sijila iliopo kata ya Pwaga na kumalizia na ukaguzi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Simbachawene katika kijiji cha Kidenge kata ya Luhundwa,ikiwa na thamani ya Shilingi 544,225,626 kutoka SEQUIP Kwa kila mradi.
Mpwapwa - Dodoma, Tanzania
Anwani: S.L.P 12
Simu: 255 26 2320122/2320
Simu ya Kiganjani: +255 688639341
Barua pepe: info@mpwapwadc.go.tz
Copyright © 2021 Mpwapwa District Council . All rights reserved.